

![]() |
|

![]() |
|
Na Calvin Gwabara, Kilosa
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imewataka Wananchi
kwenye vijiji Vinavyotekeleza Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya Vijiji
kuunga Mkono kwa dhati jitihada za Mashirika ya TFCG na MJUMITA kwa kukomesha
kabisa vitendo vya Uchomaji misitu ya vijiji ili waweze kuendelea kunufaika na
rasilimali hizo vizazi na vizazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi
Maliasili na Utalii Mhe. Ally Makoa (MB) wakati akizungumza na Wananchi wa
Kijiji cha Chabima Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kamati
hiyo ilipotembelea na kujionea na kujifunza namna Shirika la kuhifadhi misitu
ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu Tanzania
(MJUMITA) Wanavyotekeleza Mradi wa Usimamizi shirikishi wa misitu ya Jamii
(USMJ) chini ya Mradi wa kuleta mageuzi katika ya mkaa Tanzania (TTCS)
inavyofanya kazi na kulinda misitu huku ikinufaisha jamii.
“Tumeona kazi kubwa ya kutoa elimu ya utunzaji na usimamizi wa misitu ya
jamii iliyofanywa na wadau hawa lakini kiukweli bado kuna wimbi kubwa sana
uchomaji wa misitu katika wilaya ya kilosa kwenye njia ambayo tumepita tukija
kijijini kwenu, Miradi hii itakuwa na maana zaidi kama Wananchi mtashiriki
kikamilifu katika kuzuia mioto hii tuliyoiona njia nzima maana inaharibu kabisa
malengo ya Mradi na Serikali katika kutunza misitu hii muhimu kwa ustawi wa
Taifa letu”alisema Mhe. Makoa.
Amesema kwakuwa wanatambua kuwa Wafugaji ndio wanaochoma moto ameitaka
kamati ya Maliasili ya Kijiji kuongeza juhudi katika kufanya doria za kila mara
na kila siku kwakuwa fedha zinazopatikana katika biashara ya misitu inatoa
fedha za ulinzi kwa kamati kutekeleza majukumu yake vizuri hivyo nao wafanye
kazi zaidi ili kutokomeza kabisa changamoto hiyo.
Akizungumzia faida ya kuwa na misitu hiyo ya vijiji amesema kuwa inachangia
wao kupata hewa safi, Mvua ambayo inawezesha wakulima kulima lakini pia mbao na
mazao mengine ya misitu yaliyovunwa kwa njia endelevu yanachngia katika
kuboresha huduma muhimu za jamii inayozunguka misitu hiyo.
Akileza mbinu hiyo inavyofanya kazi huku akijibu baadhi ya maswali ya
Wabunge Meneja wa Mradi huo Charles Leonard mfumu huo unatelezwa baada ya
tafiti nyingi zilizofanywa kwenye nchi mbalimbali na kuonekana kufanya vizuri
nchini Zambia ambapo jamii zimeweza kutunza misitu baada ya kupata faida kwa
mtu binafasi,Vijiji na Serikali na tofauti na maeneo mengine ambayo jamii
inaona misitu ni mali ya serikali tu.
Akijibu swali la uwekano wa uchipuaji wa miti ianyokatwa amesema mfumo huo
unafanya vizuri kwenye miti jamii ya Miyombo na huchipua kwa haraka katika
maeneo matatu ambayo ni kupitia pembeni mwa kisiki,Misizi na mbegu kuota baada
ya miti mikubwa iliyokatwa kuondoa kimvuli na kuruhusu mwanga wa mbegu kuota.
Bwana Leonard amesema Mradi hauishii kwenye kutekeleza kwa maneno tuu bali
una programu nzuri ya ufuatiliaji wa uchipuaji wa miti hiyo kwenye vijiji vyote
41 ambayo inafanywa kwa kushirikiana na watafiti Kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine
cha kilimo SUA kupitia Ndaki yake ya Misitu pamoja na Taasisi ya Utafiti wa
Misitu Tanzania TAFORI ambao hutoa mapendekezo na ushauri wa namna bora ya
utekelezaji na uboresjhaji wa mfumo huo ingawa takwimu za mwaka jana zimeonesha
zaidi ya asilimia 88 mfumo umefanya vizuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa TFCG bwana Charles Lyimo amesema
Vijiji hivyo havitaishia kunufaika na Mkaa,Mbao na mazao mengine lakini pia
vitaweza kupata faida kwenye uuzaji wa hewa ya kaboni kwakuwa miti mipya
inayochipua itakuwa na uwezo zaidi wa kuvuta hewa hiyo kuliko miti ya miaka mingi
iliyozeeka.
“Mwaka 2008 tulikuwa tunatekeleza miradi 9 ya MKUHUMI kwenye Wilaya
takribani 7 kuliwezesha taifa kujiandaa kunufaika na uuzaji wa hewa ya Ukaa na
badae mkutano mmoja wa COP mataifa kadhaa yalishindwa kukubaiana katika ununuzi
wa hewa hiyo na kupelekea changamoto na kushuka kwa progamu hiyo lakini kupitia
Kaboni Tanzania ikaja ya Kiteto a Rukwa na Katavi na sasa Serikali imetengenza
kanuni ambazo sasa hata vijiji hivi vitanufaika” alifafanua Bwana Leonard.
Wakieleza namna walivyonufaika na Mradi huo Afisa mtendaji wa Kijiji kwa
niaba ya Wananchi wa Kijiji cha Chabima Bi Marrygoleth Mlengeni amesema Mradi
ulianza mwaka 2017 lakini awali mwaka 2011 mradi wa MKUHUMI uliwezesha kutengeneza mpango wa matumizi bora ya ardhi
katika Kijiji chao kwa kupanga maeneo ya mkazi,Kilimo,Misitu,ufugaji na hivyo
kusaidia katika usimamizi wa ardhi.
Amesema kupitia Mradi wa Mkaa endelevu wameweza kusimamia vyema misitu ya
vijiji na kuwezesha kununua vifaa kama vile Pikipiki kwaajili ya kufanya doria
huku Fedha hizo zikisaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kijijini
hapo ikimo Zahanati,Uchimbaji wa Choo cha Hospitali na kulipia bima ya fya CHF
Iliyoboreshwa kwa watu 100 kijijini hapo.
“Changmoto kubwa tunayokumbana nayo katika kuteleza mradi huu ni namna ya
kudhibiti moto kichaa unaochoma misitu ya hifadhi ya vijiji, Mifugo kwenye
misitu tunayoihifadhi na changamoto za migogoro ya Wakulima na wafugaji”
alifafanua Bi. Mlengele.
Shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa pamoja Wanavyotekeleza Mradi wa Usimamizi shirikishi wa misitu ya Jamii (USMJ) chini ya Mradi wa kuleta mageuzi katika ya mkaa Tanzania (TTCS) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la uswiss (SDC).
Post A Comment: