Na Mario Mgimba Njombe


Zaidi ya Wakazi 1000 wa kijiji cha Utweve Kata ya Ukwama Wilaya ya Makete Mkoani Njombe wanatarajia kuepukana na changamoto kubwa ya kupanda milima na kushuka pindi wanapotafuta maji baada ya serikali kuanza kutekeleza mradi wa zaidi  ya shilingi milioni 304.


Katika Utekelezaji wa mradi huo ambao umefikia asilimia 71  Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Makete  Mhandisi Innocent Lyamuya alisema kuwa pindi mradi huo wa utekelezaji utakapokamilika utakwenda kuwa Suluhuhisho la   tatizo la maji kwa wananchi kijijini humo.


''Dhamani ya kazi zilizofanyika ni asilimia 71 na kiasi cha fedha kilichopokelewa ni zaidi ya milioni 293 kwahiyo huduma ya upatikanaji wa maji tuna tegemea baada ya kukamilika kwa mradi huu itakuwa ni masaa 24''Alisema Mhandisi Innocent Lyamuya


Wakieleza utekelezaji wa mradi huo Wananchi wa kijiji cha Utweve Wilaya hiyo Tibery Sanga,Toba Ilomo na Christopher Sanga  wamekiri kuwapo kwa Changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji hivyo kujengwa kwa mradi huo kutawaondolea changamoto hiyo.


''tulikuwa tunafuata maji mbali na tulikuwa tunaamuka sakumina moja unaludi nyumbani saa mbili kwahiyo tulikuwa tuna beba nguo tunaenda kufulia mtoni kwa mradi huu tunaamini utapunguza changamoto hii ilikyokuwa ikitukabili muda mrefu''


Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Nchini Mhandisi Clement Kivegalo  alisema ni lazima mapinduzi ya miradi bora ya maji ianzie Makete ambako anatokea Katibu mkuu wa wizara ya maji kwani haiwezekana eneo wananchi wake wakaendelea kutaabika kwa miaka mingi.


''Nikupongeze kwa hatua mliyofikia hapa nilipo ndipo nyumbani kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji sasa Mkurugenzi wangu wa maji tuanze kuhamasisha kwa nguvu ili ikifika mwaka 2025 tayari wananchi wa Makete wana maji''


Kwa upande Diwani wa kata ya Ukwama Emmanuel Sanga amesema kilio cha maji kwa wakazi wake  kimekuwa ni kikubwa na hivi sasa furaha yao imeanza kuonekana baada ya mradi huo kufikia hatua nzuri.


''Nikweli hiki kijiji kulikuwa na changamoto kubwa ya maji kuna shule yetu ya wasichana ya makete Girls walikuwa wanaacha shughuli zao za asubuhi wanaenda kuchota kwahiyo ishukuru sana Rais  samia suluhu hassani kwa kukutuletea mradi huu''Alisema Diwani wa kata ya Ukwama Emmanuel Sanga.

Share To:

Post A Comment: