Wananchi wa kijiji cha Lemooti kata ya Lemooti kilichopo wilaya ya monduli mkoani arusha, wameishukuru serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ya afya.


Hiyo ni mara baada ya shilingi Bilioni mbili nukta saba na sitini na tatu ambazo zimeingia kwa muda wa mwaka mmoja.hata hivyo naibu waziri wa afya amesema kuna milioni hamsini ambazo zinatarajiwa kuja hivi karibuni.Waziri huyo wa afya kwa niaba ya waziri wa afya Mh.Godwini Mollel,amezindua zahanati ya afya katika kijiji hicho ambacho kipo katika kijiji cha olmooti wilaya ya monduli, ili kuweza kuondoa changamoto za umbali wa wana kijiji kupata huduma za afya na kupoteza maisha.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Mh.Fredrick Lowassa, amewataka wanakijiji hao kutumia kituo hicho kwa kuokoa maisha yao huku akiwataka kukata bima za afya ili kuweza kupunguza gharama za matibabu na kuendelea kufanya shughuli za maendeleo na kwa faida za afya zao.

Halikadhalika mkuu wa wilaya ya monduli Mh.Frank Mwaisumbe, ameishukuru serikali ya Mh.Rais Mama Samia Suluhu Hassan kupitia naibu waziri wa afya pamoja na mbunge wa monduli huku akiahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha kituo hicho kinapata wataalamu wa kutosha kuweza kuhudumia wananchi.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: