Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu yaliyoanza jana mkoani hapa..
Mkurugenzi  wa Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Batholomea Jungu, akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu yaliyofanyika mkoani hapa jana na kufikia tamati leo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada.
Picha ya pamoja. 


Na Dotto Mwaibale, Singida

MKURUGENZI  wa Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Batholomeo Jungu amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Rasilimaliwa Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa, sehemu ya Utawala  na Rasilimali Watu kushindwa kufuata Itifaki na Uratibu wa matukio ya viongozi wa kitaifa.

Jungu ameyasema hayo  jana mkoani Singida kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu.

Alisema  kuna baadhi ya Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu hawajui hata mavazi ya kuvaa pale kunapokuwa na viongozi wa kitaifa, huku wengine hawajui hata namna ya kula mbele ya viongozi wa kitaifa.

Aidha alisema mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki kwenye matukio ya viongozi wa kitaifa kwa wakurugenzi yanatajwa kuwasaidia wakurugenzi hao kujua itifaki viongozi wa kitaifa wanapofika katika maeneo yao ya utendaji.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Ezavier Daud alisema  mafunzo hayo yatawasaidia kuondoa au kupunguza changamoto zinazojitokeza katika masuala ya itifaki kwa Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu.

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba  alitoa wito kwa wakurugenzi hao na makatibu tawala wasaidizi kuyatumia mafunazo haya kuwa suluhisho la makosa yanayojitokeza kwenye suala la itifaki.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo haya wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kujua kujua itifaki Kwenye matukio ya viongozi wa kitaifa wanapotembelea maeneo yao. 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: