Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' mkoa wa Tanga  Specioza Owure akimsikiliza mfanyabiashara Wilbard Robert Mallya wakati alipomtembelea ofisini kwake leo November 23 ,2022.

Meneja wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Tanga akizungumza na meneja biashara kutoka kiwanda cha Tanga Phamarcetical& Plastic Ltd wakati aliotembelea kiwandani hapo kuzungumza nao kuhusu maswala ya ulipaji kodi.

Baadhi ya walipa kodi wa mkoa wa Tanga wakimsikiliza meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania  'TRA' mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza katika hafla ya kuwapongeza kufwatia mkoa huo ulioobika kidedea katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha uliopita  2021/2022.

 Na, Denis Chambi, Tanga

Mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' mkoa wa Tanga kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inakusudia kukusanya kodi kiasi cha shilingi Billioni 232.69 ikiwa ni malengo ya serikali sawa na ongezeko la asilimia 37 ya mwaka wa fedha uliopita. 

Hayo yameelezwa na meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati akizungumza na walipa kodi katika hafla fupi ya kuwapongeza kwa ulipaji wa kodi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 waliovuka lengo ambapo waliibuka kidedea katika mikoa yote Tanzania. 

Kutokana na ongezeko la makusanyo hayo kwa mwaka huu wa 2021/2023 meneja Owre amewataka wafanyabiashara wote mkoa wa Tanga kuendelea kushirikiana kikamilifu na mamlaka ya mapato katika kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati na kwa hiari ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na kuwezesha kufanya vizuri tena kwa mwaka huu wa 2022/2023. 

"Kikubwa ni kutoa shukrani zetu kwa walipa kodi wa mkoa wa Tanga kwaajili ya kutuwezesha kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo mkoa wetu wa Tanga tulikuwa tumepangiwa lengo la kukusanya billion 169.68 lakini tukaweza kukusanya billion 207.52 ikiwa ni sawa na asilimia 121.6% tunasema asanteni sana"

 "Tunaomba pia katika mwaka huu 2022/2023 ambapo lengo letu limeongezeka takribani billion 63 hiyo ni sawa la ongezeko la asilimia 37% lengo la mwaka huu ni billion 232.69 kwahiyo tuna kazi kubwa ya kufanya kwa sababu mwaka jana tuliweza ndio maana mwaka huu tumeongezewa lakini hatukuweza sisi wenyewe kama TRA bali nyie wadau wetu wakubwa ndio mliweza kutuwezesha mkalipa kodi kwa hiari" alisema Owure. 

"Tumekuwa tukishirikiana na kushauriana mambo mbalimbali katika jumuia zenu nafikiri kwa ushirikiano huo ndio maana ulileta mafanikio hayo makubwa kwahiyo naomba ushirikiano mliotuonyesha mwaka jana na mwaka huu muendelee na tunaweza tena kuibuka kidedea, lengo ni kubwa lakini tukishirikiana halitakuwa kubwa " aliongeza meneja huyo.

 Pamoja na hayo Meneja amewataka wafanyabishara wote kuendelea kufwata shria za ulipaji kodi pamoja na kutekeleza maagizo ya serikali ya kulipa kodi kupitia mfumo wa kielektroniki sambamba na kuwatak kutoa taarifa kwa mamlaka ya mapato pale panapotokea changamoto ywyote ikiwemo ya kusitisha biashara au kuhama. 

"Ni vyema basi wafanyabiashara wote wakalipa kodi kwa mifumo rasmi lakini pia wawe na mawasiliano na TRApale inapotokea changamoto yeyote ni vyema wakatoa taarifa inatokea changamoto mtu anafunga duka zaidi ya miaka miwili au mitatu lakini TRA hawana taarifa niwaombe kwamba wawe na mawasiliano na ofisi zetu" alisema Owure.

 Akizungumza mwenyekiti wa jumuia ya wafanyabiashara kanda ya Kaskazini Selestini Kiria ameipongeza mamalaka ya mapato kwa mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa fedha uliopita huku wakiwaomba kuzidi kuboresha huduma zao ili kuzidi kuwavutia watenda kuweza kulipa kodi kwa wawakati. 

Aidha ameomba kuendeleza ushirikiano baina ya mamlaka ya mapato na wafanyabiashara ili kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara

 "Niwapongeze kwamba mmevuka lengo na bado mmepanga kuvuka lengo mnafanya vizuri lakini muangalie na kuzilinda na bishara nyingine ndogondogo ili ziendelee kukua, lakini bado kuna changamoto kwenye utoaji wa huduma kwa walipa kodi kwahiyo tuendelee kuhimiza wafanyabiahara kuwapa huduma nzuri ili waje na hatimaye tuendelee kufanya vizuri zaidi na zaidi" 

Baadhi yao wafanyabiashara akiwemo Husseinali Hassan kutoka kiwanda cha Tanga PharmaceticalPlastic Ltd 'TPPL' pamoja na mfanyabiashara Wilbard Mallya wameiomba serikali kupitia mamlaka ya mapato TRA kuwaangalia wafanyabiashara katika suala la kodi pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma.

 " Kulipa kodi ni lazima kwa wafanyabiashara wote lazima tulipe kodi kwa muda unaotakiwa na ni jukumu letu kulingana na sheria za kodi , tunaomba TRA ituangalie wafanyabiashara wakubwa watuhudumie kwa wakati ili na sisi tuweze kufanya kazi kwa haraka" alisema Hassanali.

 "Changamoto tulizonazo ni nyingi muda mwingine unakuta wateja hamna kwa siku nzima unaweza kukusanya shilingi elfu 15000, tunaomba kupunguziwa gharama za kodikidogo " alisema mmoja wa wafanyabishara wa vyakula.
Share To:

Post A Comment: