Na Mashaka Mhando

TIMU ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA Sports Club), imejitapa kuibuka na ushindi wa jumla katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma (SHIMUTA) iliyoanza juzi Jijini hapa.

Katibu wa TRA Sports Kamna Shomari, alisema mamlaka hiyo imejipanga kuhakikisha inatwaa ushindi kila mchezo ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi wa jumla.

"Sisi TRA Sports tumejipanga kushiriki mashindano yote yaliyoandaliwa na SHIMUTA... Tutashinda michezo yote na kuibuka washindi wa jumla," alisema Shomari.

Shomari alisema wamjipanga katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete basketiball, karata, Drafti na mchezo wa Pool Table.

Hata hivyo, Shomari alisema mashindano ya mwaka huu wamejipanga zaidi kushinda mchezo wa Pool Table ambao wanataka kuchukua ubingwa wake kwa vile wachezaji wanaocheza mchezo huo, wamejipanga zaidi.

"Kati ya vikombe tutakavyorudi navyo Dar es salaam ni pamoja na kombe la Pool Table," alisema Shomari.

Shomari alisema kwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo wa Pool wameweka meza ya mchezo huo katika hotel waliyofikia kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na mshindano.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu ya TRA Sports kwa upande wa timu ya mpira wa miguu, Martin Mahimbo alisema wanatarajia kutwaa ubingwa wa mchezo huo.

"Tumecheza michezo minne, tumeshinda michezo mitatu na kusuluhu mchezo mmoja," alisema Mahimbo mchezaji wa zamani wa Coastal Union.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: