Katibu wa michezo kutoka shirika la umeme Tanzania makao makuu  'TANESCO' Stanley Uhagile        akizungumzia michezo wanayoshiriki katika mashindano ya SHIMUTA yanayoendelea mkoani              Tanga .
    Kocha wa timu ya mpira wa miguu ya shirika laumeme Tanzania  'TANESCO' Hemedi Mtumwa.

Na Denis Chambi, Tanga. 

SHIRIKA  la Umeme Tanzania 'TANSECO' mwaka huu kunako Shimuta hawataki utani buana! kwani ni wao pekee ndio ambao mpaka sasa wanaendelea kushiriki michezo yote  inayoshindaniwa huku mashiriki taasisi na makampuni mengine yakiwa yamebakiwa na mchezo mmoja mmoja. 

Tanesco wana uzoefu katika mashindano  hayo kwa miaka mitatu mfululizo tangu 2018 wakichukuwa ubingwa wa jumla wakijipanga na mwaka huu kurejesha heshima yao ambayo ilipote kwa miaka mitatu mfululizo.

Timu yao ya mpira wa miguu jana (jumatano) imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali wakiifunga  mamalaka ya afya ya mimea na viuatilifu 'TPHPA 'bao 1-0 , michezo mingine ya mpira wa wavu , kikapu pamoja na mpira wa pete wakiigia kwenye hatua ya nusu    fainali, na kwa upande wa wakimbiza upepo(Riadha) wakifanikiwa kuchukua ushindi wa mita 100, 200 pamoja na 400.

 Akizungumza katibu wa michezo kutoka Tanesco Stanley Uhagile amesema kuwa malengo yao makubwa ambayo walijiwekea tangu mwanzo wa mashindano hayo wakitekeleza pia ahadi ya viongozi wao  wa shirika ni kutaka kuchukua ubingwa wa jumla wa mahindano hayo mwaka huu wa 2022 wakijipanga kila mchezo kufika fainali . 

 "Malengo ya shirika mpaka sasa yapo palepale na  tumeendelea kupambania katika michezo yote ikiwemo michezo ya jadi lengo letu ni kuwa mabingwa wa jumla na bado  tunaendelea kuipambania"

 "Kwa hatua hii tuliyofikia mpaka sasa tunalishukuru shirika la umeme  kwa sababu wametusaidia kwa kiasi kikubwa nguvu kubwa sana tumepata kutoka kwao na tunaendelea vizuri mpaka sasa hatuna majeruhi yanayoweza kutuathiri isipokuwa wapo wachache ambao afya zao zinaimarika  kwahiyo kila kitu kinaenda vizuri, hivyo tunatoa shukrani kwa uongozi wa shirika" alisema Uhagile. 

 Kocha anayekinoa kikosi cha mpira wa miguu Hemedi Mtumwa amesema kuwa haikuwa rahisi kwao kuwatoa mamalaka afya ya mimea na  viuatilifu 'TPHPA'  kwenye hatua ya 16 bora hii ni kutokana na ushindani waliokutana nao pamoja na mechi nyingine za  tangu mwanzo lakini uimara wa kikosi chao umethibitika . 

 "Mechi haikuwa rahisi kwetu wapinzani  tuliokutana nao ilikuwa ni ngumu kuwafunga ni watu ambao wako vizuri kimwili na wanacheza mpira safi wana mwalimu anayejua mpira lakini na sisi vile vile tulijitahidi kwa uwezo wetu matokeo yake tumeweza kushinda goli 1-0 na kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali"

 "Sisi tuna uzoefu katika mashindano haya na miaka miwili iliyopita hatukufanya vizuri lakini mwaka huu tunaamini tutajipanga ziadi kuhakikisha tunavuka hadi nusu fainali ili kuweza kuchukuwa ubingwa na kurudisha hadhi yetu ambayo ilipotea kwa muda, kikubwa ni kuwaomba wafanyakazi wenzetu waendelee kutuombea na kutupa hamasa kwa kila hali ili tuendelee kufanya vizuri zaidi" alisema Mtumwa.

 Mashindano hayo yanayozushirikisha timu za watumishi kutoka mashirika ya umma, taasisi binafisi na makampuni almaarufu kama SHIMUTA  inaelekea ukingoni ikitarajiwa kutamatika November 29 kwa mabingwa wa michezo mbalimbali kujulikana. 

 Michezo inayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, Wavu, Kikapu, pamoja na michezo ya jadi ikiwemo Riadha, Bao, Draft na mingineyo.
Share To:

Post A Comment: