NA.. DENIS CHAMBI, TANGA

 Timu zinazowakilisha Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii 'NSSF' kwenye mashindano ya SHIMUTA zimeapa kuweka historia ya kufanya kwa vizuri kwenye michezo wanayoshiriki na  ikiwezekana kutwaa kombe hii ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hiyo  ya mwaka huu 2022 inayoshirikisha maahirika ya umma makampuni na taasisi binafsi. 

 NSSF ikishiriki michezo ya mpira wa miguu tayari mpaka sasa wameshashuka dimbani mara 3 ushindi mmoja na sare mbili , kwenye mpira Pete wakipoteza moja na kushinda moja huku kwenye Kikapu ikicheza michezo miwili na kupoteza mmoja wakiendelea kupambana kuhakikisha kuwa hawarudi mikono mitupu kunako mashindano hayo.

 Moja kati ya michezo iliyoshiriki na kushinda kwa ushindi mnono kwenye mpira wa Pete NSSF imeipigisha kwata timu ya DIT baada ya kuichapa magoli 51 kwa 15 mchezo uliochezwa kwenye uwaja wa Chumbageni Polisi jijini Tanga.

 Akizungumza katibu wa michezo kutoka NSSF Baome Kiwamba amesema kuwa kwa ujumla bado timu zao zinaendelea kufanya vizuri kikubwa ni kuendelea kuwaombea wachezaji wapambane ili kuhakikisha wanatimiza lengo lao la kuweka historia kwa mara ya kwanza kwenye Shimuta.

 "Pamoja na ugeni tulionao kwenye mashindano haya lakini tunajivunia kwa sababu timu zetu zinaendelea kufanya vizuri na tunategemea kufanya mazuri zaidi kwenye michezo yetu ya mpira wa miguu mpira wa pete pamoja na kikapu" alisema Baome. 

 "Cha kuwaambia wenzetu wa NSSF pamoja na viongozi ni kwamba kazi waliyotutuma tuifanye na sisi tunaifanya kama ipasavyo kwa umoja wetu tunawaahidi kwamba hatutatoka bure tumekuja kupambana ni lazima tuhakikishe tunarudi na ushindi ofisini" alisema Baome. 

 Kiwamba ambaye pia ni nahodha wa timu ya mpira wa miguu amesema kuwa licha ya wao kuwa wageni katika michuano hiyo wameweza kuhimili  mikiki mikiki ya ushindani uliopo baina ya timu pinzani wanazokutana nazo huku wakizidi kujiimarisha kuhakikisha kuwa kila mchezo kwao unakuwa ni fainali.

 "Ushindani upo na ni mzuri kuna timu nyingine zinaonyesha zimejiandaa sana licha ya kwamba ni mara yetu ya kwanza kushiriki mashindano haya lakini tutapambana ili kuhakikisha kuwa tunafika mbali na sisi tuko tayati kwa mtu yeyote ambaye tunakutana naye atakavyokuja na sisi tutajipanga kama jinsi alivyo kikubwa tutatumia madhaifu yake kuhakikisha tunamshinda" alisema.

 Michuano hiyo ambayo imeanza kutimua vumbi  mkoani Tanga tangu November 15 kwa michezo tofuati tofauti kuchezwa inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na makamu wa rais Dkt.Phillip Mpango ambaye pia ni mlezi wa Shimuta na hatimaye kuhitimishwa November 29 kwa mabingwa wa mwaka 2022 kujulikana. 

 Michezo inayoshindaniwa kwenye Shimuta mwaka huu ni pamoja na mpira wa miguu, pete, wavu, Kikapu, Draft, Dats, kukimbia kwenye magunia, kuvuta kamba , riadha pamoja na Vishale. 
Share To:

Post A Comment: