NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omar Kipanga  akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba,Tamasha la vitabu linalofanyika Jijini Tanga.
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omar Kipanga  akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba,Tamasha la vitabu linalofanyika Jijini Tanga.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza  wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba,Tamasha la vitabu linalofanyika Jijini Tanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Tanga January akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba,Tamasha la vitabu linalofanyika Jijini Tanga.


Na Oscar Assenga,TANGA

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omar Kipanga amewataka waandishi na wachapishaji wa vitabu kuandika vitabu vinavyokidhi mahitaji ya jamii ikiwemo kukuza mila na tamaduni za kitanzania Ili kuongeza wigo wa wasomaji wengi na malengo ya elimu kufikiwa.


Alitoa kauli hiyo Rai hiyo wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba,Tamasha la vitabu linalofanyika Jijini Tanga.


Alisema kuwa kwa kufanya hivyo wataongeza wigo wa wasomaji na hivyo elimu itaweza kusambaa kwa watu wengi katika jamii hali ambayo itasaidia kuongeza uwelewa wa Mila na tamaduni zetu lakini na Kujenga mapenzi ya kusoma vitabu.


"kama tunavyojua maktaba ni sehemu ya kuongeza maarifa hivyo endeleeni kuhamasisha jamii kupenda kujifunza kupitia uelimishaji wa maktaba Ili waweze kuongeza maarifa mapya kupitia usomaji wa majarida na vitabu"alisema Naibu Waziri Kipanga.


Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Tanga Omar Mgumba aliiomba serikali kuja na sera ambayo itaelekeza uwepo wa maktaba kuanza ngazi ya shule za awali Ili kutengeneza jamii inayopenda kujisomea Ili kupata maarifa mapya Kila siku.


"Wakati tunasubiri sera ni vema ngazi ya familia kukawa na chumba Cha kujisomea katika nyumba zetu Ili kujenga utamaduni wa watoto kupenda kujisomea mapema"alisema Mkuu wa mkoa.


Nae Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya huduma za maktaba Tanzania Dkt Mboni Ruzegea alisema kuwa Ili kwenda sambamba na mabadiliko ya utoaji wa huduma wanatarajia kuanza kutoa huduma ya maktaba mtandao Ili kuongeza wigo wa wasomaji na watumiaji wa huduma zao nchini.


Alisema kuwa Bado wigo wa watumiaji wa huduma za maktaba Kwa hapa nchini ni mdogo kutokana na changamoto ya kimiundombinu katika baadhi ya majengo ya maktaba hapa nchini.


"Tunaishukuru serikali Kwa kutupatia sh Bil mbili Kwa ajili ya kutengeneza mifumo ya kitaifa ya kupata huduma za kimaktaba Kwa njia ya kidijitali ambao utasaidia kusogeza huduma karibu na jamii"alisema Mkurugenzi huyo.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: