Mbunge wa Jimbo la Hanang Mkoani Manyara Mhe. Eng. Samwel Xaday Hhayuma akizungumza jambo na baadhi ya Wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Garawja , Jana Novemba 2, 2022


Mbunge wa Jimbo la Hanang Mkoani Manyara Mhe. Eng. Samwel Xaday Hhayuma akivishwa taji na mmoja wa  Wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Garawja , ikiwa kama sehemu ya kumpongeza kwa kuweza kuhudhuria mahafali hayo kama mgeni Rasmi lakini pia kumpongeza kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya katika Jimbo la Hanang.
................................................************************.........................

Na Mwandishi Wetu.

Mbunge wa Jimbo la Hanang Mhe. Eng. Samwel Xaday Hhayuma Novemba 2, 2022 amehudhuria Mahafali ya kuhitimu Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Garawja ikiwa ni mwaliko alioupata kutoka kwa uongozi wa shule hiyo , wa kumuomba ahudhurie kama mgeni Rasmi.

Akizungumza wakati wa Mahafali hayo Mhe. Hhayuma amewapongeza wanafunzi hao kwa kuweza kupambana hadi kuhitimu elimu yao ya msingi na kuwakumbusha kuwa inabidi wawe vijana wazuri huko katika jamii zao wakati wakisubiri kujiunga na Elimu yao ya Sekondari.

Aidha Mhe. Eng. Hhayuma ametumia hadhara hiyo kuelezea mikakati mizuri inayofanywa na serikali Chini ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha Elimu nchini , Ikiwa ni pamoja na Elimu kuendelea kutolewa bure , Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ya kutolea elimu kama vile Vyumba vya Madarasa n.k

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: