Na John Walter-Manyara

Vijana wenye vipaji kutoka  kanda ya Kaskazini  Manyara, Arusha, Kilimanjaro,Tanga pamoja na kanda ya kati Dodoma na Singida, wametakiwa kuwa  wabunifu na nidhamu ili kutimiza malengo yao.

Hayo yamesemwa  Novemba 14,2022  na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brand Limited David Mulokozi wakati akizindua Tamasha la kusaka vipaji linalojulikana kama (Strong Talent Search)  yaliyoandaliwa na Smile FM redio pamoja na Mati super Brand Limited kupitia kinywaji cha Strong dry Gin.

Akizungumza na vijana mbalimbali kutoka mikoa hiyo waliochukua fomu za ushiriki, Mulokozi amesema kuna vijana wengi wenye vipaji lakini wanakosa sapoti na kuishia kurekodi kwa gharama kubwa kazi zao na kuziweka katika mitandao ya kijamii bila faida,  lakini kupitia tamasha hilo wengi watafika mbali.

Amesema Platform hii ni fursa kubwa kwa Wasanii kwani watu wengi huwategemea katika  kutuliza stress zao kwa kuburudika huku wao wakiingiza kipato.

Ameongeza kuwa kwa watakaofanikiwa kupitishwa na majaji watafundwa  maadili mbalimbali ya msanii aweje na Kampuni hiyo itawasiadia kwa kila jambo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Smile Fm Redio Jamal Mteri, Mchujo wa kwanza utaanza rasmi Novemba 19, 2022 katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati.

Share To:

Post A Comment: