Na,Jusline Marco;Arusha



Zaidi ya wataalamu 50 kutoka nchi mbalimbali Duniani wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya mkataba UNESCO wa urithi wa kidunia wa asili na kitamaduni, mkataba ulioletwa mwaka 1972 na kuridhiwa na Tanzania mwaka 1977,utakaofanyika jijini Arusha mwanzoni mwa mwezi Desemba. 



Mkutano huo ambao umeandaliwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) umelenga kuipa UNESCO, nchi wanachama pamoja na wadau fursa ya kuangalia na kujadili mafanikio ya mkataba, changamoto zinazowakabili nchi wanachama pamoja na kijifunza utekelezaji wa mkataba huo kutoka kwa wadau mbalimbali.



Akizungumza katika semina ya kuelimisha wanahabari juu ya mkataba huo Mkuu wa kitengo cha sayansi asilia kutoka shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya sayansi, elimu na utamaduni  (UNESCO), Keven Robert amesema kufanyika kwa mkutano huo kunatokana na kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na umoja wa mataifa katika makubaliano ya utekelezaji wake katika usawa wa mazingira na utamaduni.



“Tanzania imepewa jukumu la kuandaa mkutano huu kwasababu ni mwanachama wa UNESCO lakini pia ni miongoni mwa nchi za mwanzo kuridhiwa mkataba huu pamoja na kuwa na historia nzuri ya kutekeleza mkataba huu toka 1977 na kufanya  kuwa nchi ya mfano kwaajili ya kijifunza ikiwa ni pamoja na kuweza kutatua changamoto zinazo tokea katika maeneo haya kwa njia ya maridhiano,” Alisema Keven Robert.



Aidha amesema pamoja na Tanzania ni mojawapo ya nchi wanachama zilizopo katika utekelezaji mzuri wenye mafanikio ikifuatiwa na  Stone Town -Zanzibar, Kilwa kisiwani na Kondoa rock art, huku ya asili ni Kilimanjaro, Serengeti na Selous pamoja na Ngorongoro ambayo maeneo hayo yaliyopo kwenye orodha ya urithi wa kidunia.



Robert amesema Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ni fursa katika kuleta nchi za kiafrika kufika nchini kujifunza namna njema walivyotekeleza mkataba huo pamoja na kubadilishana changamoto zinazoikabili ikiwemo wataalamu wa kutosha.



Kwa upande wake Kamishna Msaidizi mwandamizi wa uhifadhi kutoka mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Joshua Mwankonda amesema semina hiyo ni muendelezo wa namna ambayo mamlaka hiyo inatoa elimu ya uhifadhi, maendeleo pamoja na utalii kwa wanahabari ambapo kutokana na maadhisho hayo.



Vilevile ameongeza kuwa nchi ya Tanzania imekuwa ikinufaika na mkataba wa urithi wa asili na kiutamaduni katika kujitangaza hali inayosaidia kuongeza watalii katika hifadhi ya ngorongoro hivyo matarajio yao ni kuongeza ubora wa kiwango cha uhifadhi.

Share To:

Post A Comment: