Wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wamemchagua Mohamed Ali Mohammed (Kawaida) kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.


Kawaida ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Kusini Unguja anachukua nafasi ya Kheri James ambaye Juni 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.


Kawaida amepata kura 523 akiwashinda Farid Mohammed Haji aliyepata kura 25, Kassim Haji Kassu kura 2 na Abdallah Ibrahim Natepe aliyepata kura 1.
Share To:

Post A Comment: