Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. Gye Shul Park ambaye ni Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sung Shin Rolling Stock ya Korea (kushoto kwake) kuhusu mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakati alipotembelea karakana ya kutengeneza mabehewa ya treni inayomilikiwa na kampuni hiyo, Oktoba 25, 2022. 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania yanayotengenezwa na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock (SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini.

“Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu.”


Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Oktoba 24, 2022) mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.


Kadhalika, Waziri Mkuu amemkaribisha nchini Rais wa Kampuni hiyo Gye Shul Park aje kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mpango wa Serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli


“Mnakiwanda kikubwa, teknolojia ya hali ya juu pamoja na utaalamu na watalaam kwenye eneo hili. Kwa sasa tuna mipango mikubwa ya kuendelea kuiboresha sekta hii ya usafiri wa reli, yapo maeneo tofauti kwenye mpango wa kuunganishwa na reli ya kisasa (SGR), nakukaribisha kuja kuwekeza kitu kama hiki Tanzania.”


Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar.


Mheshimiwa Majaliwa alimshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza zaidi mpango huo na kufikia maeneo mengi zaidi.


“Mfumo huu kwasasa umekuwa wa kitaifa, ushirikishwaji wa Wananchi ni mkubwa, sasa tunataka tuikuze zaidi, haya maeneo ya Morogoro na Zanzibar tunataka yawe mifano, kwenye utekelezaji wa eneo hili”


Pia, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Ubunifu cha CEIC kilichopo kikichopo katika mji wa Pangyo
Share To:

Post A Comment: