Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mheshimiwa Anthony Mavunde ameahidi kuboresha zaidi mashindano ya Dodoma Ndondo Cup  mwaka 2023 kwa kutafuta wadau wengi kufadhili mashindano haya sambamba na ukarabati wa viwanja wa kuchezea.

Mavunde ameyasema hayo jana katika Hotel ya Royal Village,Dodoma  wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Ndondo Cup 2022 ambapo jumla ya zawadi za Tsh 11,000,000 zilitolewa kwa mabingwa,mshindi wa  pili,Timu mbili zilizoingia nusu fainali ukiacha bingwa MAJENGO SOKONI  FC na mshindi wa pili FIVE STARS FC pamoja Kikundi/Mshabiki bora wa muda wote.

“Niwashukuru wote kwa ushirikiano hasa Shaffih Dauda na timu yake yote kwa kukubali kuleta mashindano haya Dodoma,natambua pia ushirikiano uliotolewa na Hoteli ya Royal Village na Black gin katika kufanikisha mashindano haya Dodoma.

Tumeanza mwaka huu pasipo na ufadhili mkubwa,lakini nawaahidi katika mashindano ya msimuo ujao tutaboresha eneo hili kwa kutafuta wadau wa michezo kutuunga mkono,sambamba na hilo nitaendelea kukarabati viwanja vingi vya michezo hapa Jijini Dodoma ili kwa msimu ujao tuwe na viwanja vingi vinavyochezeka.

Shabaha yetu kubwa ni kuyafanya mashindano haya kuwatambulisha wachezaji kutoka Dodoma nje ya mipaka ya Dodoma na hivyo kuwa fursa kwa wao kupata Timu za kuchezea katika mashindano mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi kupitia vipaji vyao”Alisema Mavunde

Akizungumza kwa niaba ya Chama cha soka mkoani Dodoma (DOREFA) Ndugu Joseph Sehaba amempongeza Mbunge Mavunde kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta ya michezo mkoani Dodoma na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano wa kutosha katika kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wanamichezo wa Dodoma.




Share To:

Post A Comment: