Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara imekabidhi vifaa vya michezo kwa watoto wanao kuzwa vipaji vyao chini ya mwalimu Mkongwe wa mpira alimaarufu kwa jina la Mayo.

Hatua hiyo ya Halmashauri ya Mbulu imekuja baada ya kuamua kukuza vipaji vya watoto katika michezo hapa nchini hususani katika Halmashauri hiyo chini ya wizara ya Michezo, Sanaa na utamaduni ili kupata vijana watakao lisaidia taifa la Tanzania katika michezo kimataifa.

Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo ambavyo ni jezi pamoja na mipira, kwa niamba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu Mkuu wa kitengo cha Michezo, Sanaa na Utamaduni Wilayani Mbulu Ndg, Benson Maneno, Ameeleza kwamba wao kama Halmashauri ya mbulu hawata ishia hapo kusaidia watoto mbali mbali wenye malengo ya kukuza vipaji kwa madhumuni ya kujiajili katika michezo mbali mbali.

"Tutaendelea kusaidia walimu wote wanao wafunza vijana wetu michezo mbali mbali ndani ya Halmashauri yetu kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji kwa vijana ambao ndilo taifa la kesho". Alisema Benson Maneno.

"Nadhani wote ni mashahidi mnaona kazi kubwa anayo ifanya Mhe, Rais wetu Samia Suluhu Hassan ya kukuza tasnia ya michezo hapa nchini na sisi kama wasaidizi wake tuliyopo ngazi za chini lazima tuungane nae kwa pamoja kuhakikisha michezo hapa nchini inakuwa kwa kiasi kikubwa". Alisistiza Benson Maneno.

Aidha Benson alifafanua kwamba kwasasa michezo ni Ajira,Afya na ni njia sahihi kwa vijana kujiepusha kukaa katika makundi mbali mbali ya uhalifu na matokeo yake wakiwa katika kujifunza na kuendeleza vipaji vyao itawasaidia katika maisha yao na kujikuta ni wanamichezo wakubwa ndani na nje ya Tanzania.

Kwaupande wake Mwalimu Mayo aliyepokea vifaa hivyo vya michezo kwa niaba ya vijana wake alieleza kwamba aliamua kujikita kukutafuta vijana wenye vipaji kwa lengo la kuwapa njia na mwanga vijana hao ambao ndoto zao ni kuwa wanamichezo wakubwa na kwa kutambua thamani ya michozo aliona ni bora kuziamsha ndoto za vijana hao kwa kuanza kuwafundisha kabumbu.

"Niliamua kuziwasha taa za ndoto za maisha ya vijana katika michezo nikiamini siku moja watakuja kuwa wanamichezo wazuri na wakubwa katika Taifa hili, Nimpongeze sana Mkurugenzi wa Halmashauri yetu ya Mbulu pamoja na Mkuu wa kitengo cha Michezo, sanaa na Utamaduni kwa kutambua na kuthamini jitihada zetu na kuwapa vifaa vya michezo vijana hawa na niwaombe watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na michezo kuendelea kutusaidia". Alisema Mayo.


Share To:

Post A Comment: