Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC imeanzisha shule kwa watoto walio lazwa hospitalini wenye magonjwa sugu  kwa kutumia mtaala wa serikali pamoja na elimu stadi ya kumuandaa mtoto kisakolojia kabla na baada ya matibabu.


Akizindua mradi huo sambamba na kitabu maalumu cha Aisha In Hospital kilicho andaliwa na Medical Aid to Margnalised Society of Tanzania (MediamsTanzania) kwa kushirikiana na Aisha& Friends, Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC Prof Gileard Masenga amesema kuwa kitabu hicho kimebeba maudhui ya elimu stadi kuhusu maisha halisi ya mtoto akiwa hospitalini kwa matibabu ya muda mrefu.


"Hospitali nyingi hazina huduma kama hii ya kusaidia watoto kupata huduma ya matibabu kwa kufahamu nini kinacho endelea katika matibabu yake tunataka mtoto ajue kwanini anapatiwa matibabu na vitu gani vitaenda kufanyika kwa mwili wake ili kumuondoa katika msongo wa mawazo"Prof.Gileard Masenga Mkurugenzi KCMC.Aidha ameeleza kuwa tafiti zinaonesha mtoto anapokuwa na msongo wa mawazo inachelewesha uponaji wake tofauti na wasio kuwa na msongo wa mawazo ambao hupona kwa haraka hivyo programu hiyo itawasaidia watoto walio lazwa kuanzia miezi 3 na kuendelea."Watoto hao ni wale wanao ugua magonjwa sugu  kama vile saratani,moyo,kuungua na magonjwa mengine wanaotumia muda mrefu hospitalini,tunataka wapate elimu ya darasani ili waendane na wenzao walio shule pamoja na kupata elimu ya afya zao ambapo mpaka sasa zaidi ya watoto 100 pamoja na wazazi wao wamefaidika na mradi huu mpya,wanaambiwa wata chomwa sindano ili wapone pamoja na kuoneshwa mtoto wa mdoli anayepatiwa matibabu kama yake ili kumjenga kwanza kuzoea hali na kuondoa uoga" alisema Prof.Masenga.


Prof.Masenga aliongeza kusema kuwa saratani za watoto zipo na zinatibika lakini wanahitaji kupata tiba kwa muda mrefu hivyo ni vema wakapatiwa masomo ya darasani kipindi chote wanapatiwa huduma ili kuwaondolea msongo wa mawazo na kujiona wanasoma kama wenzao.


"Tunapata watoto wengi wanao tibiwa saratani hapa KCMC na ni bila malipo na kwa mwaka hospitali inasamehe zaidi ya shilingi bilioni 5 kwaajili ya tiba za saratani kwa watoto,tuna jenga hosteli maalum kwaajili ya wazazi na watoto wanao subiria matibabu ya saratani".Prof. Masenga


Awali akitoa taarifa ya mradi huo wa  KCMC Hospital Hope School, Daktari John Minja Mwanafunzi wa udaktari bingwa wa magonjwa ya ngozi na zinaa  (KCMC) ambaye ni Kiongozi shirika la Medical Aid to Margnalised Society of Tanzania amesema kuwa mradi huo ulio anza mwaka 2019 ni mahususi katika kusaidia watoto kisaikolojia pamoja na kuwapa wazazi na watoto hao vitabu vya msaada wa jamii katika hisia."Tunataka kutengeneza mazingira rafiki kwa mtoto katika hospitali,kumfundisha kutambua na kuweza kuongelea hisi zake na kupunguza msongo wa mawazo ili kupona haraka" alisema  Minja.


Aliongeza kusema kuwa mradi huo umepokelewa vizuri na wazazi wanaohudumia watoto hospitalini hapo kwani na wao wanapata elimu ya kuwaondoa na msongo wa mawazo.


"Huwa ni wakati mgumu kwa familia na mtoto pale inapobidi apelekwe hospitalini,mtoto anakuwa ameondolewa kwneyet mazingira aliyoyazoea na kuyaamini ili kwenda kufanyiwa vipimo na kupata matibabu,kipindi hiki anapo kuwa mgonjwa mtoto huwa na maumivu mengi na pia anakosa nafasi ya kwenda shule" aliongeza Minja.


Akishukuru kuanzishwa kwa mradi huo,Miriam Ibrahimu mzazi anaye muhudumia mtoto wake mwenye saratani ameeleza kuwa mradi utawasaidia katika kuwa rudishia matumaini yaliyo potea.


"Unajua tunatumia muda mrefu kuuguza hospitalini kama mzazi unapata msongo wa mawazo watoto wengine wapo nyumbani peke yao bila mama au niliye naye hospitali anakosa masomo ya darasani hivyo mradi huu utasaidia sana mtoto akipona akirudi shule anaendelea na masomo darasani,tunaahukuru MediamsTanzania" alisema Miriam.

Share To:

Post A Comment: