Na Theophilida Felician Kagera.



Waziri wa  ofisi ya waziri Mkuu, kazi, vijana, na wenye ulemavu Prf Joyce Ndalichako amefika Mkoani Kagera kuangalia hali ya maendeleo ya maandalizi ya maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge zitakazo hitimishwa Mkoani Kagera mnamo tarehe 14/10/ mwaka huu wa 2022.



Waziri Ndalichako akiwa katika viwanja vya shule ya msingi kashai Manispaa ya Bukoba kunakoendelea na mazoezi ya halaiki kwa vijana kutoka shule mbalimbali za msingi amesema kwamba katika maadhimisho hayo mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani.


 Hata hivyo amewapongeza  vijana wa halaiki hiyo na wa kufunzi wao chini ya mkufunzi Mkuu halaiki Taifa Kilema Athumani kwa jinsi wanavyoendelea kwa kasi kubwa  katika kufanya mazoezi mbalimbali kama alivyoyashudia kwa macho viwanjani hapo. 



Amewasihi vijana hao kuhakikisha wanayazingatia kwa umakini maelekezo wanayoekelezwa na wakufunzi wao.



Hata hivyo akiambatana na uongozi wa Serikali ya Mkoa ameyatembelea na maeneo mengine ya takayohusika na sherehe  hazo  vikiwemo viwanja vya Kaitaba, huku akiwaelekeza  viongozi hao wa mkoa kuunganisha nguvu  kwa pamoja zaidi ili maadhimisho hayo yaweze kufana na kuwa mfano kwa mikoa mingine.

Share To:

Post A Comment: