Na John Walter-Manyara

Gari la dharula la TANESCO mkoani Manyara limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katika Mlima wa Logia wilayani Babati mkoani Manyara na kusababisha vifo vya wafanyakazi watatu wa Shirika hilo na wengine watatu kujeruhiwa

Akitoa Taarifa hiyo Afisa uhusiano wa TANESCO mkoani hapo Marcia Simfukwe amesema kuwa wafanyakazi hao ambao ni mafundi umeme wamepata ajali hiyo wakiwa wanaelekea Dareda kufanya Matengenezo ya miundombinu ya Umeme

Chanzo cha ajali hiyo ni Lori lililokuwa lilishuka katika mlima huo kufeli breki na kugonga gari la shirika hilo

Wafanyakazi waliopoteza maisha ni Yona Nashon , Ramadhani Madenge na Bura Nyoka ambao wanatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Kwaraa wilayani Babati

Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma kwa Matibabu zaidi.

Share To:

Post A Comment: