Na Karama Kenyunko 


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepokea kama kielelezo hati ya upekuzi na mapazia 23 yanayodaiwa kufanafanana na pazia moja linalodaiwa kufungia mwili wa marehemu Farihani Maluni aliyeuwawa na kufukiwa mbele ya nyumba huko Ilala Sharif Shamba, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Uamuzi huo umefikiwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Minde, baada ya aliyekuwa mpelelezi Deusdedit Chenga kuiomba mahakama ipokee hati hiyo kama kielelezo katika kesi ya mauaji inayomkabili Hemed Ally.

Mapema, akitoa ushahidi wake shahidi Chenga amedai kuwa hati ya upekuzi ilifanyika nyumbani kwa mke wa mtuhumiwa mtaa wa Faru karibu na Faya, Dar es Salaam baada ya mtuhumiwa kutaja mapazia mawili aliyoyatumia kufanyia mauaji ya Maluni.

Alidai katika mapazi hayo mawili moja alimzika nalo na lingine lilichomwa moto na mapazia 23 alihamishia kwa wazazi wa mke wake

Amedai, walikwenda kufanya upekuzi wa mapazia hayo ambayo yanafanana na yale aliyodumbukiza katika shimo alilomfukia Maluni baada ya kumuua.

Tuliongozana na mke wa mtuhumiwa hadi nyumbani kwao
baada ya kumzuia alipoenda kituo cha polisi Msimbazi kumpelekea mtuhumiwa Ally chakula.

Chenga amedai alikwenda nyumbani kwa mkwe wa mtuhumiwa akiwa na mke wa mtuhumiwa ambapo kabla ya kuingia ndani aliitwa mwenyekiti wa mtaa huo ambapo walijitambulisha na kisha kumueleza kwamba walifika kwa ajili ya kielelezo cha mapazia.

Baada ya kujitambulisha alituruhusu kuingia ndani ya hiyo nyumba ya familia ambapo tuliingia moja kwa moja hadi chumbani cha mke wa mtuhumiwa tulikuta sanduku tukafungua tulikuta pazia moja la rangi ya gold akadai zingine ziko stoo na ufunguo hana ilibidi kuvunja.

Baada ya kuvunja waliingia ndani ambapo katika upekuzi waliona mfuko wa plastiki juu ya kabati na walipoufungua walikuta jumla ya mapazia 23 ambayo waliyajaza katkka hati ya upekuzi na kusaini wao pamoja na Mwenyekiti kisha wakarudi kituoni Msimbazi.

Awali, kabla ya kupokelewa kwa hati ya upekuzi, upande wa utetezi walipinga kielelezo cha mapazia yasipokelewe kwa sababu hayakufuata taratibu za kukitoa kielelezo hicho Mahakamani hapo kwamba hakutoa hati ya upekuzi

Hakimu Joyce aliahirisha kesi hiyo hadi leo na mshitakiwa alirudishwa rumande,

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka inadaiwa Juni mwaka 2014 Hemed Ally aanatuhumiwa kumuua Farihani Maluni eneo la Sharif Shamba ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.


Share To:

Post A Comment: