Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Shukuru Musabila kulia akimkabidhi vifaa vya Michezo shule ya Msingi Gofu juu aina ya mabembea yenye thamani ya Milioni 13.5Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Perpetua Mhina  kwa ajili ya makuzi ya watoto wanaosoma darasa la awali kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Gofu Juu Monica Joseph

 -

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Shukuru Musabila kulia akimkabidhi vifaa vya Michezo shule ya Msingi Gofu juu aina ya mabembea yenye thamani ya Milioni 13.5Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Perpetua Mhina  kwa ajili ya makuzi ya watoto wanaosoma darasa la awali kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Gofu Juu Monica Joseph
Sehemu ya wanafunzi wa darsa la awali katika shule ya Msingi Gofu Juu Jijini Tanga wakiwa kwenye mabembea hayo mara baada ya kukabidhiwa -yaliyotolewa na Shirika la Brac Maendeleo Tanzania 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Shukuru Musabila  akizungumza mara baada ya kumalizika makabidhiano hayo
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Perpetua Mhina  akizungumza ambapo aliishukuru Shirika la Brac Tanzania kwa kuwasaidia msaada huo
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Gofu Juu Monica Joseph akizungumza


Sehemu ya watumishi wa Shirika la BRAC Tanzania wakiuwa wamekalia bembea hilo kabla ya kulikabidhi
Hapa wakiwa kwenye picha za pamoja mara baada ya makabidhiano hayo


Na Oscar Assenga,TANGA.

TAFITI zilizofanywa zinaonyesha  watoto wanaokuwa majumbani wasiochanganyikani na wengine katika vituo vya malezi na makuzi wamekuwa na tatizo la udumavu ambalo limepelekea  utambuzi wao kuwa ni hafifi .

Hayo yalisemwa na   Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Shukuru Musabila wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa vya Michezo shule ya Msingi Gofu juu aina ya mabembea yenye thamani ya Milioni 13.5 kwa ajili ya makuzi ya watoto wanaosoma darasa la awali.

Alisema kwa maana hawawezi kutambua kitu kutokana na umri wao lakini wanapokuwa kwenye vituo wanakuwa na malezi mazuri na makuzi ya utambuzi wa kisaikoloji na kiakili unakuwa mzuri zaidi kumjenga na kuweza kumuandaa kikamilifu.

"Nitoe wito kwa wazazi na malezi kuendelea kuwabaini watoto wote ikiwemo wenye ulemavu kwenda kwenye vituo vya malezi huku akisisitiza kwamba wanakabidhi vifaa hivyo kwa vile  vinapatikaba kwa jamii" Alisema 

Aidha alisema kwamba wataendelea kufanya kazi na Serikali na wadau wengine kuhamasisha hasa kwenye malezi na makuzi ya watoto ili baada ya mradi kwisha ili wazazi na walezi waweza kuchukua nafasi yao ya kuchangia gharama za ukarabati wa vifaa na chakula.

Shukuru alisema wamekabidhi vifaa hivyo kwa shule ya awali iliyopo  katika kituo cha  shule ya Msingi Gofu Juu Kata ya Nguvumali ikiwa ni muendelezo wa jitihada zao  za kuwasaidia watoto hapa nchini walioanza mwaka 2006.

Alisema kwamba mradi huo kwa  Tanzania una maeneo makuu matatu mojawapo ikiwa ni kuwasaidia kuwezesha wazazi na walimu  elimu ya makuzi ya watoto ambao wana miaka  kati ya mitatu hadi mitano .

"Tulianza kwa mikoa ya Mbeya,Dar na sasa tumefikisha katika mikoa ya Tanga na Dodoma na maeneo mengi nchini lengo lao ni kuwafikia watoto katika maeneo mbalimbali katika malezi na makuzi ulinzi na mtoto na katika eneo hili tunafanya kazi na  Serikali kupitia wizara ya Maendeo ya Jamii,Wanawake na Makundi Maalumu kuandaa kiongozo cha malezi ya watoto chini ya miaka mitano " Alisema 

"Kwa namna hiyo leo wanakabidhi vifaa vya michezo kwa shule ya Gofu Michezo lakini hiki ni moja ya vituo 20 vilivyopo Tanga na vyengine zipo Korogwe na maeneo mbalimbali hivyo nitoe wito kwa wazazi sisi kama Brac Maendeleo Tanzania tumeweza kuwafikia watoto hao wakiwa kwenye vituo hivyo lakini wazazi tunawaita ili kuweza kuendelea kuwapa ulinzi watoto hao maana wanapokuwa wakiwa kwenye kituo wanakuwa na ulinzi .

Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Perpetua Mhina alitoa shukrani kwa Shirika la Brac Maendeleo  Tanzania kwa namna wanavyoendelea kusaidia katika sekta ya elimu na kwa makuzi kwa watoto .

Perpetua alisema  mabembea hayo yatasaidia kukuza vipaji vya watoto  kama lengo lao kauli mbiu yao inavyosema kujifunza kwa vitendo hiyo wanaamini kupitia uwepo wake utakuwa kichocheo cha kuwasaidia hata watoto wasiopenda shule  akiyakumbuka atakuwa hawezi kukosa shule na hivyo kupunguza hata utoro

Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Gofu Juu Monica Joseph alisema kwamba wanalishukuru Shirika la Brac Tanzania kwq namna wanavyopeleka miradi ya maendeleo kwenye shule hiyo na kituo hicho kimekuwa ni chachu kwao kwa ajili ya kupata watoto wanaojiunga na darasa la awali kwa ajili ya kujiunga na darasa la kwanza.

Hata hiyo alitoa wito kwa wazazi na Jamii kushirikiana naa kuweza kulinda vifaa vinavyoletwa ili watoto waweze kujifunza zaidi huku akieleza kwamba changamoto kubwa ni kwamba shule hiyo haina uzio hivyo watu mbalimbali wanaweza kupita bila ruhusa.

"Hivyo  tunaomba wadau watusaidie kuweka uzio kwenye shule hii ili vifaa vinavyopelekwa shule hiyo viweze kuwa salama"Alisema

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: