Na Ahmed Mahmoud

Watendaji wa mahakama kutoka nchi za ukanda wa Afrika wametakiwa
kuzingatia uhuru wa vyombo vya habari  na usalama wao katika utoaji wa
sheria na misingi yake kwa lengo la kuhakikisha waandishi wa habari
wanauhuru wa kutoa habari.

Akizungumza kando ya mafunzo ya watendaji wa mahakama juu ya uhuru wa
kujieleza na usalama wa waandishi wa wanahabari yaliyoandaliwa na
shirika la elimu,sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa(Unesco)
,Rais wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu  na watu,Jaji Imani
Abudi  alisema lengo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanayo haki ya
kuandika habari pamoja na kusikilizwa.

"Uhuru wa vyombo vya habari na usalama wao ni jambo muhimu sana kwani
waandishi wa habari ni watu muhimu katika  jamii yoyote ambayo
inaheshimu juu ya utawala wa sheria,demokrasia na haki za
kibinadamu,"alisema Jaji Abudi.

Alisema kupitia mafunzo hayo yatasaidia kupata elimu namna vyombo vya
utoaji haki kutoka Afrika vinaweza kutumika kwa njia bora ya kuweza
kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanakuwa na uhuru wa kutoa na
kupewa habari pamoja na kusikilizwa kwa kuzingatia usalama wao.

"Pia Majaji watafundishwa  namna njema ya kushughulikia mashauri
yanayohusu wanahabari kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi
mbalimbali zilizopo Afrika hivyo nasisitiza kuwa namna mahakama ya
haki za kibinadamu na wanatu inavyotoa  maamuzi yake
mbalimbali,"alisema Rais huyo.

Alisisitiza kuwa mahakama za nchi katika umoja wa Afrika wanaweza
kushirikiana  katika kubadilishana uzoefu kwenye maamuzi na mambo
mengine yanahusiana na masuala ya wanahabari pamoja na haki zao.

Aidha alisema ni vyema wanahabari wa nchi za Afrika wakawa wazalendo
katika kulipoti matukio mbalimbali yanayohusu bara la Afrika ili
kudumisha amani kuepuka kwa kuzingatia usalama wao.

Kwa upande wake Rais wa mahakama ya jumuiya ya Afrika ya
mashariki(EACJ), Nestory Kayobera alisema katika kipindicha miaka 20
wameshapokea kesi mbalimbali zaidia ya 170 ambapo kila mwananchi
kutoka nchi mwananchama anahaki ya kufungua kesi bila masharti yoyote.

Naye David Ngunyale ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo alisema
mafunzo hayo ni muhimu kwao katika kujengewa uelewa kwani kwa
kushindwa kufanya hivyo itawapelekea kushindwa kufanya kazi na watu
wengine wakiwemo waandishi wa habari.

"Kwa hiyo kwa msingi mkubwa wa mafunzo haya ni kwa ajili ya utawala wa
sheria unavyohusianishwa na uhuru wa kutoa habari,"alisema.

Mkuu wa mradi wa uwajibikaji wa wanahabari kutoka UNESCO Mehdi
Benchelah alisema kuwa uhuru wa kujieleza imekuwa ni changamoto kubwa
Duniani ambapo kumekuwa na kesi nyingi za wanahabari  wakati mwingine
wanauwa jambo linaloathiri tasnia nzima ya habari na wananchi kwa
ujumla kwa kukosa uhuru wa kupata habari.

"UNESCO tumeona ni vyema kuwapa mafunzo haya watendaji wa mahakama ili
kuwapa uelewa juu ya utawala wa kisheria na uhuru wa kujieleza ambapo
wanapadishana mawazo ni vipi nchi za ulaya na za Afrika zinavyofanya
katika kuhakikisha uhuru wa habari unakuwepo na kuweza kusimamia suala
hili,"alisema Benchelah.

Mmoja wa wanahabari aliyehudhuria mafunzo hayo,Lucas Miyovela alisema
ni vyema wadau hao wakaanza kuwashirikisha waandishi wa habari moja
kwa moja  ili waweze kufahamu changamoto zinazowakabili.




Share To:

Post A Comment: