Amani Mongi : Arusha 

Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela ameliagiza jeshi la polisi mkoani hapo kuhakikisha vishkwambi vitano vilivyoibiwa kipindi cha sensa vinapatikana kwa matumizi ya umma.

Akizungumza septemba 8,2022 wakati wa utoaji wa taarifa za sensa ya mwaka huu iliyoanza Agasti 23 na kukamilika Septemba 5,2022,Mongella amesema jumla ya vishkwambi vilivyoibiwa  vilikuwa nane na vitatu vikapatikana hivyo ni vyema jeshi la polisi awakavisaka vilivyobaki kwa ajili ya matumizi ya umma.

"Jeshi la polisi muhakikisha  vishkwambi vitano vilivyopotea vinapatikana haraka iwezekanavyo kwa ajili yamatumizi mengine ya umma na msizembee kisa sensa imeisha,"amesema Mongela.

Awali akitoa taarifa ya sensa hadi kukamilika kwake,Mtakwimu mwandamizi Ofisi ya Taifa ya takwimu,Omary Maulid amesema jumla ya kaya 5383488 na majengo 568720 yameweza kufikiwa katika mkoa wa Arusha.

"Pamoja na mafanikio hayo pia kulikuwepo na changamoto ya wizi wa vishkwambi,upatikanaji wa mtandao wakati wa kuandikisha watu na makazi kuhusu taarifa zao,"amaesema Maulid.

Aidha amesema awamu inayofuata ni kuchambua taarifa  na ifikapo Oktoba mwishoni ,Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ataweza kutoa matokeo ya awali ambayo yataonyesha jumla ya idadi ya watu na makazi nchini kuanzia ngazi ya kimkoa hadi Kitaifa.

Share To:

Post A Comment: