Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko (katikati) akikata utepe kuashiria upokeaji wa magari mawili yaliyotolewa na Shirika la la Elizabeth Glaser Pediatic Aids Foundation (EGPAF) kupitia Mradi wa USAID Afya Yangu Northern  yenye thamani ya zaidi ya Milioni 91.9 kwa ajili ya kusaidia usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za afya mkoani hapa. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa shirika hilo, Dk. Fredrick Haraka,  Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo, Dk. Sajida Kimambo, Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick na Mkururgenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedeki Humbe

Furaha ikitawala wakati wa hafla hiyo.


Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akijaribu kuendesha gari baada ya kukabidhiwa.
Mkururgenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedeki Humbe, akijaribu kuendesha gari baada ya kukabidhiwa.
Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo, Dk. Sajida Kimambo, akitoa taarifa ya shirika hilo.
Taarifa ya utendaji kazi ya shirika hilo ikitolewa kabla ya makabidhiano ya magari hayo.
Utambulisho ukifanyika.
Viongozi wa shirika hilo wakisiliza taarifa ya shirika hilo.
Mkurugenzi wa Utafiti wa shirika hilo, Dk. Fredrick Haraka, akijitambulisha.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika hilo, Martin Mfikwa akijitambulisha.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji wa shirika hilo,Jacquesdol Masawe akijitambulisha.
Wajumbe mbalimbali wakisikiliza taarifa kabla ya hafla ya kukabidhi magari hayo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick akizungumza.
Taswira kabla ya kukabidhi magari hayo.
Muonekano wa magari hayo.
Baadhi ya madaktari wakisikiliza taarifa kabla ya hafla ya kukabidhi magari hayo.
Hafla ya makabidhiano ya magari hayo ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Picha ya pamoja baada ya hafla ya makabidhiano ya magari hayo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SHIRIKA la Elizabeth Glaser Pediatic Aids Foundation (EGPAF) kupitia Mradi wa USAID Afya Yangu Northern  limetoa magari mawili Mkoa wa Singida yenye thamani ya zaidi ya Milioni 91.9 kwa ajili ya kusaidia usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za afya mkoani hapa.

Akizungumza  wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo, Dk. Sajida Kimambo alisema  magari hayo yatazisaidia timu za usimamizi wa huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya hivyo yatachagiza kasi na ufanisi wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi .

Alitaja gari hizo kuwa ni Toyota Land Cruiser DFP 6673 yenye thamani ya kiasi cha Sh.42,250,334/= itakayo kwenda kwa timu ya usimamizi wa afya ngazi ya mkoa (RHMT) na gari aina ya Nisssan Pick Up DFP 9272 yenye thamani ya kiasi cha Sh. 49,433,008 kwa ajili ya timu ya usimamzi wa afya halmashauri ya  Wilaya ya Manyoni na kuwabei ya manunuzi ya magari hayo ni za mwaka 2010.

Akizungumzia utendaji kazi wa shirika hilo katika kipindi cha robo mwaka tatu za utekelezaji wa Mradi wa USAID Afya Yangu Northern Dk.Kimambo alisema  mradi huo Kanda ya Kati na Kaskazini, ulianza Mwezi Novemba mwaka wa Jana, (2021) na unajikita katika afua za mapambano ya UKIMWI/VVU, Kifua Kikuu Lakini pia uzazi wa mpango, na mapambano dhidi ya UVIKO-19.

“Mradi huu umekua ukifanya kazi kwa mashirikiano makubwa na serikali kupitia wizara za afya na TAMISEMI, pamoja na timu za usimamizi wa huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya, katika mikoa sita ya Arusha, Dodoma , Kilimanjaro, Manyara, Tabora na hapa Singida na kuwa upo katika wilaya 44 na vituo 588 na kwa Mkoa wa Singida upo katika halmashauri zote saba na vituo themanini na tisa” alisema Dk.Kimambo.

Alisema mradi huo umepanga shughuli za afya katika Mkoa wa Singida kwa mwaka wa fedha 2022/2023 zenye Jumla ya Sh. Millioni mia saba ishirini na tano, laki nne, sitini na nane elfu mia nne na sitini. (725,468,460 TZS) na kuwa pesa hizo zote zitakwenda moja kwa moja katika halmashauri na tayari zimekwisha anza kutolewa katika halmashauri hizo ,RHMT na Hospitali ya Mkoa kwa awamu.

Kimambo alisema mradi huo pia umepanga kutoa zaidi ya million mia nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kutoka makoa makuu ya Taasis hiyo , hivyo kufanya thamani ya jumla ya bilioni moja za kitanzania kutoka katika shirika hilo kwenda  Mkoa wa Singida kwa mwaka 2022/2023.

Aidha Kimambo alisema kuwa  mradi huo umetoa vifaa nane vya matibabu ya viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi viitavyo thermos coagulation machine vyenye thamani ya Sh.Mmillion mia moja ishirini (120,000,000/=TZS), ambavyo vipo vituoni tayari vikiendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Alisema mradi huo pia umeweka mifumo ya TEHAMA katika vituo vya afya kwa ajili ya kutunza kumbukumbu (data management systems) ambapo kompyuta mpakato 21 na zile za mezani 34 zilinunuliwa na kufungwa katika vituo vya afya 40 zenye thamani ya zaidi Sh.116.7

Pia alisema  mradi huo una saidia usafirshaji wa sampuli za binaadamu kutoka vituo vyote mkoani kupitia mkataba na shirika la Posta na kampuni ya TUTUME, kwa kila Mwezi kulipia wastani wa kiasi cha shillingi million ishirini na tano na kuwa unalipia gharama za vipimo vya wahisiwa wa kifua kikuu wanaopaswa kupatiwa vipimo vya mionyo, lakini vipimo cha biochemistry kwa wateja wakifua kikuu sugu na wateja wa dawa kinga za VVU.

Alisema katika kutambua changamoto za akidi isiyo timilifu ya watumishi wa afya katika vituo vya kutolea huduma za afya, mradi wa USAID Afya Yangu kwa kushirikiana na Afya endelevu umeajiri watumishi wa kanda mbali mbali za afya wapatao sabini na moja (71) katika vituo mbali mbali vya afya  mkoani Singida na kuwa pia unawezesha watoa huduma ngazi ya jamii wapatao mia mbili sabini katika vituo mbali mbali ili kuchagiza utoaji wa huduma za afya katika jamii.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akipokea magari hayo alisema yaende yakatumike kwa kazi iliyokusudiwa na kuwa atakuwa mkali katika kuyasimamia na watu watamuona mbaya katika usimamizi wake.

Mkururgenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,  Melkzedeki Humbe alilishukuru shirika hilo kwa msaada huo na kuwa gari walilopewa litafanya kazi kwa ajili ya timu ya usimamizi wa afya katika halmashauri hiyo na si vinginevyo.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: