Ferdinand Shayo Manyara. 


Kampuni ya Mati Super Brands Limited iliyoko mkoani Manyara imetoa msaada kwa wafungwa wa gereza la Wilaya ya  Babati ikiwemo Magodoro ,blanketi pamoja na vifaa vya kufanyia usafi ikiwa ni njia mojawapo ya kushirikiana na serikali kuboresha mazingira kwa wafungwa . 


Akikabidhi msaada  huo Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited Doreen Raphaeli amesema kuwa msaada huo unalenga kutatua changamoto za wafungwa pamoja na kuboresha mazingira yao. 


Doreen ameyataka makampuni na taasisi mbali mbali kujitokeza kusaidia wafungwa kwani ni sehemu ya jamii ambayo inahitaji msaada wa kila mmoja. 


Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Babati Acp Nkonge Mwakatage amepongeza juhudinza kampuni hiyo zinazoenda sambamba na agizo la Raisi Samia Suluhu Hassan la kuwataka wakuu wa magereza kiboresha mazingira ya wafungwa. 


"Niwashukuru sana Mati Super Brands Limited kwa Moyo wa ukarimu na Upendo kwa ndugu zetu wafungwa ambao wapo huku kwa lengo la urekebishaji tabia kisha watarudi uraiani baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao" Anaeleza Mkuu wa Magereza. 

Share To:

Post A Comment: