Na,Jusline Marco:Moshi

Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais menejiment ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe.Deogratus Ndejembi amewataka wahitimu wa mafunzo ya awali ya uchunguzi ya taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa maafisa uchunguzi na wachunguzi wasaidizi  kufanya kazi kwa weledi,uadilifu na uzalendo.

Mhe.Ndejembi ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo hayo katika chuo cha kipolisi Tanzania Mjini Moshi na kuwataka maafisa hao kulinda na kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili ziweze kutumika kama zilivyoelekezwa kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuweka kipengele maalum cha ajira kitakachowaelekeza waajiriwa katika taasisi hiyo kuitumikia si chini ya miaka 5 kabla ya kuomba uhamisho kuelekea kwenye taasisi nyingine za umma.

"Serikali imewekeza fedha nyingi takribani bilioni 2 kwa ajili mafunzo hayo hivyo sitegemei kuona baada ya kupangiwa vituo vya kazi mnaomba uhamisho kuelekewa kwenye sekta nyingine za umma."alisisitiza Ngejembi


Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Salimu Hamduni katika hafla hiyo amesema wahitimu hao watakwenda kupunguza tatizo la upungufu wa ikama na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu,sheria,haki na ueledi ns kuelelezo bora kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurudin Babu amewataka wahitimu watapangiwa vituo vya kazi katika Mkoani wake kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kusaidia kupambana na vitenfo vya rushwa ndani ya Mkoa wake.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: