Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limezindua kampeni kupanda miti inayojulikana kwa jina la STAMICO  na Mazingira At 50 ili kuhamasisha  utunzaji wa Mazingira  na kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuhifadhi mazingira. 


Kampeni hii imezinduliwa  katika mkutano  wa Waandishi wa habari uliofanyika  leo Agosti 2, 2022 jijini  Dar es Salaam ikiwa ni moja ya shughuli itakayofanyika kuelekea maadhimisho ya Miaka 50 toka Shirika kuanzishwa kwa Shirika la Madini


Akiongea kuhusu kampeni  hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse  amesema kampeni hii imebeba kaulimbiu ya Panda Mti, tumia Mkaa Mbadala Rafiki Briquettes, okoa Mazingira na itazinduliwa tarehe 10 mwezi Agosti 2022 katika eneo la Ipagala jijini Dodoma" alisisitiza Dkt. Mwasse.


Amesema STAMICO inatarajia kupanda miti 10,000 ambapo kwa awamu ya kwanza itapandwa miti 100 katika jiji la Dodoma na baadaye katika maeneo mengine ambapo STAMICO inaendesha miradi yake.

 

Amesema, lengo ni kushiriki kikamilifu katika zoezi la kutunza uoto wa asili na kuleta hamasa ya kutunza mazingira ili shughuli za uchimbaji madini rafiki kwa mazingira.

 

Zoezi hili linafanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Ofisi ya Mkoa na Wilaya  Dodoma, TAWOMA, TFS, na viongozi wa vikundi vya mazingira, vikundi vya wanawake katika mazingira.


Ametoa wito kwa watu wa Dodoma  kushirikiana na STAMICO  katika zoezi hili la upandaji  miti.

 

Sambamba na kampeni hiyo STAMICO inatarajia 

kutoa vifaa kwa wachimbaji viziwi waliopo Nyakafuru Geita, na

kutembelea Wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean road na kuzindua bidhaa ya Makaa mbadala Rafiki Briquettes ambayo itakapofika siku ya  maadhimisho hayo.

Share To:

Post A Comment: