Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka akimkabidhi nyaraka  Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Risemary Senyamule.

Na Janeth Raphael

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary SENYAMULE amewataka watumishi wote wa Mkoa wa Dodoma kumpa ushirikiano katika utendaji kazi Ili kuleta maendeleo huku akimtaka Kila mmoja kutimiza wajibu wake kama dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassani anavyotaka mabadiliko kwa Tanzania hivyo lazima  Dodoma uwe Mkoa wa mfano.

Rosemary ametoa kauli hiyo  Leo Jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kuendeleza Mkoa wa Dodoma katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo zilizokuwa zikifanywa na Mh Anthony Mtaka.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Anthony Mtaka amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ataendelea kufanya kazi kwa uadilifu na matamanio yake ni kuhakikisha Elimu na uchumi vinakuwa juu ili kuondokana na umaskini.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fatuma Mganga ameahidi kumpa ushirikiano Mkuu huyo mpya wa Mkoa wa Dodoma ambaye ametokea Mkoa wa Geita kwa lengo la kuleta maendeleo ya Mkoa na Nchi kwa ujumla.
Share To:

Post A Comment: