Tumepokea malalamiko ya mgonjwa kuhusu kipimo cha mfumo wa chakula kuchelewa.

Malalamiko haya ni ya kweli na ya msingi. Tunavyo vifaa (scopes) 13 ambapo kati ya hivyo 9 viliharibika tumepeleka Marekani kwa matengenezo makubwa na 2 ni mpya zimepelekwa Nairobi kwa ajili ya matengenezo kinga (PM) kwa sababu hapa nchini hakuna mtaalamu anayeweza kuvitengeneza.

Hivyo kwa sasa vifaa vinavyofanya kazi ni viwili. Tunategemea ndani ya siku 7 hadi 10 vitakuwa vimerejea nchini ili kuendelea kutoa huduma.

Wagonjwa 30 wanahitaji huduma hii kwa siku na mgonjwa mmoja anatumia kati ya dakika 45 hadi saa moja na nusu (dakika 90) kutegemea na aina ya kipimo au matibabu anayopewa.

Kifaa hicho kikitoka kwa mgonjwa kinafanyiwa usafi aina tatu ambao huchukua takribani dakika 20, usafi wa awali (pre-cleaning) ili kumkinga mtoa huduma na mgonjwa, hatua ya pili husafishwa kwa maji na sabuni na badaye kinasafishwa kwa kutumia dawa (sterilization) na kisha kukaushwa kabla ya kwenda kwa mgonjwa mwingine. Hatua hii ni uzingatiaji mkubwa wa kudhibiti maambukizi (IPC) ni lazima ifuatwe.

Tunaomba radhi kwa wagonjwa kutokana na usumbufu wanaoupata, tuna hakika ndani ya siku saba huduma itarejea katika hali yake ya kawaida.

Imetolewa na

Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Share To:

Post A Comment: