Na Fredy Mgunda, MsumbaBlog


Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa  imefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa Mapato yake ya ndani kwa zaidi ya Asilimia 100 ambayo walikuwa wamejipangia kwa mwaka wa fedha unaoishia mwezi June 30.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Festo Mgina amesema wamefanikiwa kuvuka lengo la kukusanya Asilimia 126 ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Watalaamu na Madiwani hao.

"Tumefanikiwa kufikia Asilimia 126 kwa sababu ya ushirikiano mzuri uliopo baina yetu hivyo nichukue fursa hii kuwapongeza Madiwani wenzangu na wataalamu kwa juhudi kubwa  ambayo wameionyesha ya ukusanyaji wa Mapato hadi kufikia Asilimia hizo." Amesema Mgina

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa  wafanyabiashara wamekuwa wanalipa  ushuru  ambayo ndio mapato ya halmashauri kwa Moyo Mmoja halo ambayo imesaidia kuweza kuvuka kwa Lengo ambalo walikuwa wamejipangia.

Pia Mwenyekiti huyo amezungumzia namna ambavyo wataweza kukusanya mapato kwa mwaka ambao umeanza licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali  jinsi watakavyoweza kukusanya mapato hayo.

" Changamoto iliyopo kwa mwaka huu  wa fedha  ambao umeanza  namna ambavyo wafanyabiashara  hawajitumi kulipa kodi kwa ihari  kwa sababu mfumo wa ukusanyaji wa ushuru wa mapato ya ndani umekuwa na mabadiliko kutokana na sheria  ambayo imebadirishwa na bunge na kuletwa utaratibu mwingine  wa ukusanyaji wa Mapato hayo kutoka Asilimia 0.5 hadi 0.3." amesema Mwenyekiti huyo.

Amesema mabadiliko hayo yamekuwa wakati tayari makisio ya bajeti ijayo imeshapitishwa hivyo imekuwa changamoto kwa halmashauri hiyo  huku akieleza namna ambavyo wamejipanga kuhakikisha wanakusanya mapato hayo kama walivyokusudia.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itandula Iddi Mabena amesema kuwa uchumi wa Halmashauri hiyo inategemea mazao ya misitu hivyo kuvuka kwa lengo hiyo ni kutokana na jinsi ambavyo walikuwa wamejipanga.

"Malengo haya yalikuwa kukusanya zaidi ya Asilimia 126 ama zaidi ya hapo lakini hata hapo tulipofikia bado sio mbaya ila tunaimani tunaweza kwenda mbele zaidi ya hapo ili kuhakikisha halmashauri unapata mapato Makubwa na kufanya vitu vyao vya msingi ambavyo wamejipangia."amesema Mabena 

Share To:

Post A Comment: