Naibu waziri wa utamaduni Sanaa na Michezo Paulina Gekul ambaye pia ni Mbunge wa Babati mjini akikimbia Kilomita 5  mbio zilizopewa jina la Manyara Tanzanite International  Marathon  mjini Babati mapema leo Agosti 13,2022  zilizoanzia uwanja wa Kwaraa na kuzunguka eneo la kwa kastuli hadi uwanjani hapo. (Picha na John Walter).

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange  akikimbia  mbio za Kilomita 5 Manyara Tanzanite International  mjini Babati mapema leo Agosti 13,2022 , Pembeni kulia  ni Naibu waziri Utamaduni,Sanaa na Michezo (MB) Paulina Gekul  (Picha na John Walter).



Wananchi mbalimbali waliojitokeza leo agosti 13,2022 kushiriki mbio za kilomita 5 zijulikanazo kama Manyara Tanzanite International zilianzishwa na Mbunge wa jimbo la Babati mjini ambaye pia ni Naibu waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Paulina Gekul. (Picha na John Walter).




Mshindi wa Kwanza mbio za Kilomita 21 katika mbio za Manyara Tanzanite International Marathon, Elisha Wema aliemaliza mbio hizo kwa saa 1:05, leo mjini Babati.

Wema amekabidhiwa zawadi ya shilingi laki tatu na Fulana ya Mazoezi na Naibu waziri wa utamaduni Sanaa na Michezo.(Picha na John Water).

........................................................................

Na John Walter-Babati

Naibu waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo (Mbunge wa Jimbo la Babati mjini) Paulina Gekul  leo Jumamosi agosti 13,2022 ameongoza zaidi ya wakimbiaji 100 kushiriki Mbio za Manyara International Marathon 2022, ambako Elisha Wema na Neema Sanka  wote wa Babati  walitawazwa vinara wa kilomita 21 wanaume na wanawake.

Mbio hizo zilizoanzia na kuishia Viwanja vya Kwaraa zimeandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Paulina Gekul na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji ya Bonite ambao wametoa fulana za mazoezi kwa washindi wote wa kilomita 10 na 21.

Paulina Gekul  alishiriki mbio za Kilomita 5, alikowaongoza viongozi kadhaa, akiwemo mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange,Mkurugenzi wa mji wa Babati AnnaFissoo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Abdulrahman Kololi,Katibu tawala wilaya ya Babati Khaliphan Matipula.



 

Share To:

Post A Comment: