Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amefanya kazi nzuri iliyopelekea bei ya mafuta ya kula nchini kushuka.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 5, 2022, Mbalizi mkoani Mbeya, wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.

"Tulikuwa tuna tatizo kwenye mafuta yote ya aina mbili, mafuta ya kula tumeshafanyia kazi Waziri wa Kilimo amefanya kazi nzuri mafuta ya kula yameshuka bei," amesema Rais Samia

Share To:

Post A Comment: