Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliye kuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne imeahirishwa tena hadi Sept.12.2022 hadi pale ushahidi utakapo kamilika.


Sabaya na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Agosti 29, 2022 ambapo wanakabiliwa na mashitaka saba ikiwemo la uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu pamoja na kujihusisha na vitendo vya rushwa.


Kwa upande wake Wakili wa serikali anaye wakilisha Jamhuri Sabitina Mcharo  ameieleza Mahakama hiyo kuwa ushahidi bado hauja kamilika hivyo kuomba muda hadi Sept.12 mwaka huu.


Aidha wakili upande wa Washtakiwa Hellen Mauna amesema kuwa ikiwa shidaa ni kibali watalazimika kuomba shauri hilo likasikilizwe Mahakama kuu kwani washtakiwa wanaendele kuteseka magereza bila kujua hatima yao.


Akiahirisha kesi hiyo hadi Sept.12.2022Hakimu Mkadhi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi Salome Mshasha  amedai kuwa hoja zilizotolewa na upande wa utetezi ni zamsingi na muda wa kusikiliza shauri hilo umeenda hivyo upande wa Jamhuri ufanye kazi zao vizuri ili wananchi wawe na imani na  Mahakama

Juni Mosi, 2022, Sabaya na wenzake wanne walipandishwa mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kusomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.


Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.







Share To:

JUSLINE

Post A Comment: