JAJI mkuu wa Mahakama kuu ya Tanzania Profesa Ibrahimu Juma amesema kuna haja ya kuweka utaratibu wa kila Jaji wa Mahakama ya Rufani kumaliza idadi fulani ya mashauri kwa kila mwaka kwa lengo la kujipima ili kuondoa mlundikano wa mashauri mahakamani.


 


Jaji Prof. Juma alisema hayo jana kwenye Mkutano wa nusu Mwaka wa Majaji wa Mahakama ya Rufani uliofanyika mjini hapa ambapo alisema kwa Mahakama ya Rufani hawakuweka kiwango isipokuwa walitumia utaratibu wao wa muda mrefu tangu mwaka 1979 ambao kila kinapoketi kikao cha Mahakama ya Rufani kinapaswa kumaliza mashauri yote yanayopangwa katika kikao husika isipokuwa kama kuna sababu zisizozuilika za kutokumaliza shauri husika ambapo pia hawakufikia malengo.


 


Alisema takwimu zinaonyesha kuwa Mahakama ya Rufani ina mashauri ya muda mrefu 611 na mashauri 42 yanayosubiri kusomwa hukumu yaliyozidi siku 90 na kwamba licha ya vikao vya mashauri vinavyofanywa na jopo la majaji inapaswa kila Jaji anayeandika hukumu baada ya kukubaliana na wenzake ahesabiwe kwamba yeye ndiye aliyemaliza shauri hilo.


 


Alisema vigezo vya kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani vinalenga kushusha mlundikano hadi asilimia 0.05 ambapo tayari wamefanikiwa kushusha kwa asilimia 0.15 na kwamba lengo kuu ni shauri liwe mahakamani ndani ya siku 350 wakati tayari wamefanikiwa kwa sababu shauri linadumu Mahakamani kwa siku 338 ambazo ni bora zaidi ya lengo la siku 350.


 


Hata hivyo alisisitiza Majaji kuendelea kujipanga katika matumizi ya teknolojia ya Tehama ili kuboresha utoaji huduma na kufikia safari ya Mahakama Mtandao hapo mwaka 2025 kwa sababu Mhimili wa Mahakama tayari unao msingi wa uwekezaji mkubwa wa kutumia teknolojia hiyo.


 


Prof. Juma alisema faida ya matumizi ya Teknolojia ya Tehama ilionekana wazi wakati wa janga la UVIKO-19, pale Mahakama ilivyoweza kutumia teknolojia na kufanikiwa kupata hati safi ya asilimia 108.68 mwaka 2020 ambayo ni asilimia kubwa kuliko asilimia 98 ya mwaka 2019.

Alizitaja faida nyingine kuwa ni matumizi makubwa ya mahakama mtandao yaliyowezesha kushughulikia migogoro inayoletwa Mahakamani kwa njia ya haraka na kwa ufanisi mkubwa zaidi.


 


Aidha alisema kadri miundombinu ya majengo inavyosogeza huduma kwa watu wengi zaidi mashauri yataongezeka na rufani Mahakamani zitaongezeka.


 


Alisema dalili za mashauri kuongezeka mahakamani zinaonekana kwa wingi wa mashauri yanayosajiliwa kwa njia ya Mtandao kwa saa 24 ambapo kwa sasa asilimia 20 ya mashauri yanayosajiliwa kwa njia ya Mtandao ni kati ya 95 na 100.


 


Prof. Juma alisema vituo vyote vya Mahakama za Wilaya, Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama Kuu vimeunganishwa na huduma za mtandao ambapo Majengo Jumuishi 6 tayari yameanza kutoa huduma.


 


Alisema chini ya mkakati wa kidigitali wanatarajia kubadilisha utaratibu wa kupeleka mavitabu makubwa mahakamani kwa ajili ya rufaa na badala yake watatumia Teknolojia kwa kutuma vitabu hivyo kwenye mifumo ya Mahakama ya Ki-tehama ili vifanyiwe kazi.
Naye Jaji Mahakama ya Rufani Augustine Mwaliga alisema kikao hicho kimekaa mwaka 2022 baada ya kutofanyika kwa miaka miwili mfululizo kutokana na janga la Uvico-19 na kwamba licha ya ugonjwa huo mahakama


MWISHO….

Share To:

Post A Comment: