Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amemshukuru waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa kwa kufanya ziara ya ukaguzi na kisha kuweka mawe ya msingi ya chuo cha mafunzo ya ufundi Veta pamoja na hospital mpya ya wilaya ikungi na kutembelea kituo cha afya Iglanson 


Mhe. Muro amesema ziara ya waziri imeleta faraja kwa wananchi wa ikungi kutokana na maelekezo yaliyotolewa na waziri mkuu majaliwa yanayokwenda kukamilisha miradi yote ya maendeleo ikiwemo hospital mpya ya wilaya  na kituo cha afya Iglanson na chuo cha veta ambavyo amevitembelea


Dc Muro amesema kwa upande wao wanajipanga pamoja na uongozi wa halmashauri na veta kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa waziri mkuu majaliwa ndani ya muda mfupi ili wananchi wapate huduma bora za kijamii


Share To:

Post A Comment: