Na Oscar Assenga,TANGA.
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo imepokea msaada
wa maabara ya kisasa ya kufanyia uchunguzi wa ugonjwa wa Uviko 19 yenye thamani
ya Milioni 225 kutoka kwa Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika lake la
Maendeleo ya GIZ
Akizungumza mara baada ya kuifungua mara baada ya ukaguzi
wa maabara hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema kwamna maabara hiyo ina
uwezo wa kutoa majibu ndani ya masaa nane hivyo kuwa mwarobaini wa changamoto
zilizokuwepo awali.
Alisema kuwa pia kupitia uwepo wa maabara hiyo utasaidia
hata wananchi kutoka nchi jirani ya Kenya ambao wataingia nchini kufanyiwa
vipimo kwa haraka na majibu kupatikana kwa wakati.
Alisema uwepo wa maabara hiyo itaondoa changamoto
iliyokuwepo ya kusafirtisha sampuli kwenda kwenye maabara nyengine ambapo
ilikuwa inasababisha ucheleweshwaji wa majibu na wakati mwengine vipimo
vilikuwa vinachelewa.
"Kwa niaba ya serikali tunawashukuru wenzetu wa
Ujerumani kwa kutusaidia katika sekta ya Afya kama mnavyofahamu hospitali hii
ilijengwa na wajerumani miaka 100 iliyopita lakini bado wanaendelea kutoa fedha
nyingi katika kusaidia sekta ya afya nchini ikiwemo hospital yetu ya rufaa ya
mkoa wa Tanga Bombo wanatupatia fedha kwaajili ya kuimarisha afya ya uzazi ,mama
na mtoto pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona "Alisema
Alisema kuzinduliwa kwa kituo hicho cha kupima sampuli za
Corona kitasaidia na kuokoa muda kwani awali ilikuwa inawalazimu sampuli
zinazochukuliwa hospital Bombo kwenda kupimwa Dar es salaam kwenye maabara ya
Taifa na baada ya masaa 48 ndio majibu kupatikana ambapo sasa majibu yatakuwa
yanapatikana ndani ya masaa 8 na kuwarahisishia wanaosafiri kwenda nje ya nchi
kupata majibu kwa haraka zaidi.
Waziri Ummy alisema pia fedha walizitoa zitatumika kwaajili
ya kuimarisha mapambano dhidi ya Uviko -19 na ndio maana katika hospitali ya
rufaa ya mkoa Bombo wamefungua kituo cha kupima sampuli za Corona kwa kutumia
kipimo hicho.
Awali akizungumza Waziri wa Ushirikiana wa Uchumi na Maendeleo
kutok Serikali ya Ujerumani Dkt Barbel Kofler alisema kuwa wakazi wa Tanga pamoja
na wageni kutoka nje sasa wataweza kutumia maabara hiyo kwa ajili ya vipimo vya
UVIKO.
Alisema wanajisikia furaha kuona kituo hiki cha kupimia
sampuli za Covid 19 kinaanza kufanya kazi kwaajili kuimarisha afya ya jamii ya
watu wa Tanga na ni muhimu sana kwa serikali ya ujerumani kuendelea kusaidia
sekta ya afya katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
Alieleza kwa sababu wote hatuko salama muda wowote hivyo
wanapaswa kushirikiana kusaidia katika kuimarisha afya ya jamii kwa ujumla kwa
Tanzania na ulimwengu mzima pia
Dkt. Kofler alisema mbali na fedha hizo wamesaidia
kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika kutoa huduma bora huku wakingia Dolla
za kimarekani 15.3 kwaajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto na wasichana ili
kupambana, kupunguza au kutokomeza kabisa vifo vitokanavyo na uzazi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa maabara kuu ya Taifa
ya Afya ya Jamii Medard Beyanga alisema
kuwa Serikali inaendelea kuziimarisha
maabara zote hapa nchini kwaajili ya kupelekea huduma karibu na wananchi
ambapo baadhi ya vituo hapa nchini vimeanza kufunguliwa ikiwemo kilichopo katika hospital ya rufaa mkoa wa Tanga Bombo.
Alisema kwamba hivi sasa wanaendelea na mpango wao wa
kuziimarisha maabara za upimaji wa Uviko
- 19 na Serikali inafanya jitihada za
kuongeza upimaji ili kupeleka
huduma karibu na wananchi kuliko kusubiri majibu kutoka Dar es salaam kwenda
maabara kuu ya Taifa ,na hii maabara haitakuwa ya kupima Corona bali itapima na
magonjwa mengine.
Aidha alieleza pia Serikali ya Ujerumani pia imeendelea
kuwa na mchango mkubwa hapa nchini kupitia sekta ya afya ambapo inasaidia
kulipia bima ya afya na mtoto inayotambulika kama 'Tumaini la mama', kuchangia
mapambano dhidi ya kifua kikuu pamoja na malaria.
“Serikali ya Ujerumani imedhamini miradi ya afya ya
Nchini Tanzania kwa gharama ya shilingi dola za kimarekani za zaidi ya shilingi
bilioni 7 ikihusisha miradi ya mama na mtoto na Uviko 19”Alisema
Post A Comment: