Viongozi mbalimbali wa jumuiya ya Chama cha Mapinduzi kutoka kata zote za wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza leo wamepewa mafunzo wa kuwajengea uwezo katika kusimamia Ilani ya CCM, Elimu ya Sensa pamoja na jinsi ya kufaidika na 10% ya mikopo kutoka Halmashauri.


Mafunzo hayo yameratibiwa na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dr Angeline Mabula na kuhudhuriwa na viongozi wote wa jumuiya za Chama cha Mapinduzi ngazi ya Kata 19 za waliochaguliwa hivi karibuni.


Akifungua mafunzo hayo, mbunge wa jimbo hilo, Dr Angeline Mabula amewaasa viongozi hao wa CCM  kufanya kazi kwa juhudi katika kusimamia Ilani ya Chama na kumsaidia Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.


"Uchaguzi umeisha sasa makundi yavunje, nyinyi wote ni viongozi wa Chama cha Mapinduzi na sio chama kingine. Tufanye kazi kwa ushirikiano katika kutatua kero mbalimbali za wananchi kama Ilani ya Chama inavyosema".


"Mimi ndio Mbunge wenu na hayupo mwingine mpaka 2025, mimi nafanya kazi na wote na sina ubaguzi wowote. Tufanye kazi tuwe suluhisho la matatizo ya wananchi ili wafaidi matunda ya Serikali yao kupitia Chama cha Mapinduzi chini ya Amri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan" alisema Dr Mabula.


Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mheshimiwa Hassan Masala amesema kama wilaya wako macho kutekeleza majukumu ya wananchi kila siku kwa kuongozwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.


"Tumefanya kazi kubwa pamoja katika kuwahudumia wananchi wa wilaya yetu, hakuna maendelezo yatakuwa kama hakuna maelewano. Tukipendana na kuondoa yasiyo na maana katikati yetu Ilemela yetu itasonga mbele kwa spidi kubwa sana" 


"Kama wilaya tuna mkakati wa kuondoa chanagamoto zilizoko katika Wilaya yetu, tumeanza na madawati na tunaendelea kuhakikisha tunajenga vyumba vya madarasa na nyumba za waalimu" 


"Najua tunaelekea kwenye Sensa ya watu na makazi tunaomba viongozi wote wa Chama na Serikali tuhusike kuwapa wananchi Elimu ya Sensa na faida za wao kushiriki katika Sensa hiyo ya 23 Agosti 2022" alisema Dr Masala.


Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Jumamosi 7 Agosti 2022 kuanzia saa 2 Asubuhi katika ukumbi wa Monarch Hotel Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.

Share To:

Post A Comment: