Na, Moses Mashalla,

Waziri wa Nishati  nchini ,January Makamba amesema serikali inaamini Utekelezaji wa majukumu na uendeshaji  wa Shirika la  Maendeleo la Petroli nchini (TPDC),utaleta tija na maendeleo nchini hususani kwenye sekta ya Gesi na mafuta.


Makamba amesema hayo wakati akizindua bodi ya wakurugenzi wa Shirika la TPDC  Jijini Arusha na kueleza kwamba uteuzi wa bodi hiyo unaakisi dira na Malengo mapya ya serikali kwa shirika hilo kuelekea katika Mapinduzi ya sekta ya mafuta na gesi.

Amesema bodi hiyo chini ya Mwenyekiti wake Balozi Ombeni Sefue inakidhi nafasi ya TPDC katika maendeleo ya nchi, dira na mwelekeo mpya wa TPDC katika uchumi mpya wa Gesi na maendeleo ya mafuta nchini kwa ujumla.
"Dhamira yetu ni kuona Shirika hili linataoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na sio katika mapato tu Bali uendeshaji wa Rasilimali watu katika tasnia hii lakini pia ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na Gesi"alisema Makamba 


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya TPDC Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu amesema wao kama bodi kazi yao ni kwenda kuchangamsha na kuhakikisha kila kitu kinaenda inavyotakiwa ili Taifa liweze kunufaika na Rasilimali zake za mafuta na Gesi. 

"Mikakati iliyopo kwa Sasa ni ile ya serikali na haijaanza Leo tutaipitia kama bodi mpya tumefanikiwa wapi na changamoto ni zipi na zitatatuliwaje ili kazi iendelee vizuri kujenga TPDC yenye kusaidia serikali"alisema Balozi Sefue 

Awali Mkurugenzi wa Shirika la TPDC nchini James Mataragio amesema kuwa pindi miradi mbalimbali ya mafuta na Gesi itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto za wananchi na kuleta maendeleo mbalimbali nchini. 

Amesema kwa  Sasa TPDC Ina miradi mikubwa ikiwemo Mradi wa kujenga Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga hapa nchini  ambao umeonyesha mafanikio pia Kuna mradi wa kutafuta mafuta katika bonde la ufa ambao upo kwenye Mchakato. 

Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa mafuta na Gesi nchini (PURA),Mhandisi Charles Sangweni alisema kwamba uundwaji wa bodi ya TPDC utaleta tija na kusaidia shughuli za Utekelezaji ndani ya serikali na kuongeza kuwa shughuli nyingi hapo awali kama maamuzi ndani ya PURA zilikwama Kutokana na kukosekana kwa bodi hiyo.Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: