Asila Twaha, Dar es Salaam


Timu ya Tamisemi Queens  imeendelea  kuwa  tishio kwa kuonesha  mabavu yake  kwa kuichapa timu ya UDSM goli 65 -14 katika mpira wa netiboli.


Mechi hiyo iliyochezwa leo majira ya saa tatu asubuhi katika uwanja wa ndani uliopo uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ikiwa Tamisemi Queens inaendelea kuwanyoosha wapinzani wake tangu walipoanza mchezo huo.


TAMISEMI  iliendelea kuicharaza UDSM na kushindwa  kufurukuta  huku wachezaji wa timu hiyo kubanwa  na kukosa pa kuhemea kwa uwingi wa goli walizochapwa.


Wachezaji wa upande wa TAMISEMI   GK- Mecklina Lucas, GD-Merisiana Kinzenga na WD Asha Rashid kuhakikisha kunakuwa na ulinzi mkali  wa kutokupelekwa kwa goli katika lango la Tamisemi Queens.


Mpaka mchezo unafikia mapumnziko Tamisemi Queens ilikuwa inaongoza goli 33 na kwa upande wa UDSM ikiwa imepata goli 10.


Aidha, mpaka mpira unaisha Timu ya TAMISEMI  Queens ilikuwa imeshinda goli 65 UDSM ikiwa imepata goli 14.

Share To:

Post A Comment: