Na John Walter-Babati

Unywaji wa pombe aina ya Gongo imekuwa ikitajwa mara nyingi kuangamiza nguvu kazi ya taifa ambao ni vijana.

Pombe hiyo ambayo inaonekana ikinyewa maeneo ya vijijini na mijini huwaathiri watumiaji kwa njia mbalimbali na kupelekea hata vifo.

Tunajua jinsi ilivyo vigumu kudhibiti matumizi ya pombe hiyo kwani mara nyingi utengenezaji wake  ni kwa njia za kificho.

Katika mazingira kama haya, haiwezekani mamlaka za serikali kufuatilia matengenezo na uuzaji wake kwa lengo la kukakikisha kuwa watumiaji wanakunywa kinywaji safi na salama kwa afya zao.

Kwa kutambua kuwa gongo siyo kinywaji rafiki na salama kwa afya, ndiyo maana hairuhusiwi kisheria kutengenezwa na kuuzwa.

Matukio mengi yamekuwa yakionyesha kuwa gongo ni sumu kwa afya kutokana na kutengenezwa bila kuwa na vipimo ambapo Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwake kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao amepiga marufuku upikaji wa pombe haramu ya Gongo na kutoa agizo kwa uongozi wa kijiji cha Imbilili kuwakamata wapigaji na wanywaji.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Imbilili kata ya Sigino alisema gongo ni hatari kwa kuwa inapunguza nguvu kazi ya taifa ambao ni vijana.

Amemtaka mtendaji wa mtaa kukagua katika mtaa wake  kusaka nyumba zinazipikwa gongo na kuiharibu mitambo ikiwa na pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.


Share To:

Post A Comment: