MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji akisisitiza jambo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga -Pangani Saadani kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na kushoto aliyevaa miwani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Isaya Mbenje

 

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji akisisitiza jambo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga -Pangani Saadani kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na kushoto aliyevaa miwani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Isaya Mbenje
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) Mhandisi Zuhuru Amani  akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Mbunge wa Jimbo la Pangani kulia ambaye pia ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Mbunge wa Pangani (CCM) na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto akikagua  ujenzi wa barabara ya Tanga -Pangani wakati wa ziara yake leo kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  na Katibu wa Waziri Gibson George

Sehemu ya ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea
Mbunge wa Pangani (CCM) na Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika akitembelea ujenzi huo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Hassan Nyange kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo





NA OSCAR ASSENGA, PANGANI.

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kufanikisha ujenzi wa Barabara ya kutoka Tanga-Pangani –Saadan huku akieleza kwamba utawala wake umekuwa ni suluhu ya matatizo ya watanzania na wana Pangani .

Amesema ujenzi wa barabara hiyo utakapokamilika utalifungua jimbo hilo kiuchumi na hivyo kusaidia wananchi kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kimaendeleo kutokana na uwepo wake.

Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua na kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga –Pangani-Bagamoyo kwa kiwango cha lami lenye kilomita 256.

Huku akiridhishwa na kasi ya utekelezaji wake unavyokwenda huku akiwahaidi ushirikiano wakandarasi wanaotekeleza mradi huo ili kuhakikisha ujenzi huo unakwenda kama ulivyopangwa.

Alisema kwa sababu wilaya ya Pangani walikuwa na na changamoto ya barabara na wapo ambao walikuwa hawaamini kwamba ujenzi huo utafanyia lakini leo ujenzi unaendelea.

“Wapo ambao walikuwa hawaamini kwamba ujenzi wa barabara hii utajengwa lakini leo hii hapa inajengwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu tunamshukuru sana kwa hili kubwa alilotufanyia sisi wana Pangani”Alisema Mbunge Aweso.

Aidha aliwataka wana Pangani wachangamkie fursa za ujenzi wa mradi huo wa barabara kwa kuongeza uzalishaji zaidi kwa kutumia ardhi iliyopo kwa ajili ya kilimo ikiwemo kuwataka kuacha kuuza maeneo yao kiholela,

“Niwaombeni ndugu zangu sasa ujenzi huu unafanyika hii ni fursa na maendeleo kwa sababu itafungua fursa za kiuchumi hivyo niwasihi acheni kuuza ardhi kiholela holela kwa kuhakikisha mnayasimamia kutokana na fursa za kiuchumi zitafunguka wakati ujenzi huu utakapokamilika na kuweza kupata maendeleo”Alisema

Alisema kwa sababu ujenzi wa barabara hiyo unakwenda kuitoa Pangani pangoni na kuiinua kiuchumi na hivyo kufungua fursa za kimaendeleo hivyo wananchi hakikisheni mnaongeza uzalishaji.

“Niliwahi kupiga magoti hapa kuomba barabara hii lakini naishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa kutufuta machozi wana Pangani kwa kuliona hili na utekelezaji wa mradi huu kwa sasa unaendelea na kubwa zaidi unakwenda pamoja”Alisema

“Nimeanza kukagua eneo la Choba nimeridhika sana na utekelezaji wake nifikisheni salamu za pongezi kwa Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa na Watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) kwa kuwapata wakandarasi wazuri wanafanya kazi vizuri”Alisema

Aliongeza yeye kama mbunge wa Jimbo la Pangani aliwahaidi wakandarasi hao kwamba watawapa ushirikiano kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati huku akiwaeleza kwamba changamoto ambazo aliwaeleza atakwenda kukutana na Waziri wa Ujenzi kuona namna ya kuzipatia suluhu”alisema

Hata hivyo aliwapongeza Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) mkoa wa Tanga kutokana na kwamba wanafanya kazi nzuri hasa juu ya usimamizi na ufuatiliaji wa mradi huu.

“Rais Samia ni Rais wa nchi nzima lakini ametambua kiu ya wananchi wa Pangani miaka ya nyuma ukitaka kwenda Pangani kutoka Tanga unacheza kiduku mpaka unafika Pangani kutokana na miundombinu mibovu ya barabara lakini ujenzi huo utaondosha changamoto hizo”Alisema.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) Mhandisi Zuhuru Amani alisema ujenzi wa barabara ya Tanga –Pangani kilomita 50 uligharimu kiasi cha Sh. bilioni 66.853 ambayo ilikuwa ni gharama za awali lakini imeongezeka na sasa kuwa Bilioni 67.458 kutokana na mabadiliko ya usanifu,

Mradi huu ulipangwa kukamilika Novemba 14 mwaka 2021 lakini kutokana na sababu mbalimbali za kimkataba mufa wa kukamilika kwa mradi huo umeongezwa hadi Desemba 5,2022 na kazi hiyo inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.

Alisema mradi huo mwanzoni ulikuwa ukisimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S TECU (TANROADS Engineering Consulting Unit) hadi Desemba 5 mwaka 2020 na kwa sasa unasimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S Dotch LTD ya Tanzania kwa gharama ya Sh.Bilioni 2.246 na utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimai 42.3 na hadi sasa mkandarasi amelipwa hati nne za madai zenye jumla ya Sh.Milioni 8,

Alisema awamu ya pili ya mradi huo ni ujenzi wa daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525 utahusisha ujenzi wa barabara ya maungio ya daraja yenye kilomita 14.3,barabara ya mchepuko ya kwenda ushongo kilomita 5.9 na barabara za Pangani mjini zenye urefu wa kilomita 5.4.

Mhandisi Zuhura alisema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkataba umesainiwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroad) na Mkandarasi M/s Shandong Luqiao Group Co.Ltd kutoka Chini Mei 5 mwaka huu kwa gharama zaidi Sh. Bilioni 82 kwa muda wa miezi 36 ya ujenzi na miezi 36 ya kipindi cha uangalizi kwa upande wa daraja ni miezi 12 kwa upande wa barabara.

Hata hivyo alisema kwa upande wa barabara ya Tungamaa –Mkwaja-Mkange kwa kiwango cha Lami (Km 95.2) ikijumuisha na barabara ya mchepuko ya Kipumbwi yenye kilomita 3.7 unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mradi huo ulishasainiwa na mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchini.

Alisema na mkandarasi M/s China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G) kutoka china kwa gharama za zaidi ya Sh.Bilioni 94 na kwa sasa muda wa miezi 36 ya ujnzi na miezi 12 ya kipindi cha uangalizi na kazi ya ujenzi imeanza Aprili Mosi mwaka huu na inatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 31 2025 na zaidi ya Bilioni 14 zimelipwa kwa mkandarasi na mpaka sasa ikiwa ni malipo ya awali ya Mhandisi Mshauri kuidhinisha malipo hayo na utekelezaji wake umefikia asilimia 5.1.

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: