Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),Emmanuel Humba Akipata maelezo Wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH katika maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam Mapema leoAfisa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH akitoa Maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),Emmanuel Humba

Na Ahmed Mahmoud


Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuel Humba amesema kuwa kama Taifa la Tanzania linataka kuendelea na kuendana na mabadiliko ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ipo haja ya kuwashika mkono na kuwasaidia vijana wanaobuni bunifu zenye tija kwa Taifa ili waweze kufanya makubwa zaidi.


Humba aliyasema hayo, Leo Julai 6, 2022  alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Sayansi  na Teknolojia (COSTECH) katika Maoenesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba ambapo aliwapongeza wabunifu hao na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwawezesha Vijana kutangaza bunifu zao kwa watanzania.


Amesema kuwa amevutiwa na kijana aliyebuni dawa za tiba mbadala zinazotengezwa kwa kutumia sumu ya nyuki pamoja na kijana aliyetengeneza mashine ya kuchenjua dhahabu.


Akihitimsha ziara yake fupi katika Banda la COSTECH Bw. Humba alitoa wito kwa Watanzania wote kwa pamoja kuwashika mkono vijana hao ili wafanye makubwa zaidi kwa faida ya Taifa la Tanzania.


#Sabasaba #COSTECHTanzania #Ubunifu


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: