Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akipokea Mkuki kutoka kwa Askari wa Jeshi la Akiba mbele ya mnara wa Mashujaa ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Mashujaa Mapema Leo Jijini Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiteta Jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Pindi Chana na Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mussa Matoroka Mapema Leo Jijini Arusha

Na Ahmed Mahmoud 

Mavetenari waliopigana  Vita vya Kagera leo wameadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kuweka silaha za jadi kwenye bustani ya Mnara wa Mashujaa Jijini Arusha.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana sambamba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe,viongozi wa dini pamoja na wananchi.

Akizungumza mara baada ya uwekaji wa silaha za jadi ikiwemo ngao,mkuki,shoka na sime,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mongella alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo ndani ya nchi kwakuhakikisha wanalinda amani na kudumisha mashikamano. 

Naye Luteni Mstaafu,Allais Robert ambaye aliwahi acha nafasi yake ya uhasibu na kwenda kupigana vita vya Kagera mwaka 1978 hadi 1979,alisema wakati alipokuwa akienda vitani alikuwa na hamasa kubwa ya uzalendo wa nchi.

Alisema alipokuwa akienda kupigana vitani alikuwa na umri wa miaka 24 na alikuwa tayari kuendana na hali halisi ya mazingira waliyokutana nayo vitani.

"Wakati wa vita tulipata msaada kutokana kwenye vikosi mbalimbali vya majeshi yetu kutoka vyuo mbalimbali na tulijitoa kwa hali na mali kupigania nchi yetu na kumng'oa Nduli Idd Amin "

Alitoa rai kwa vijana kutokimbilia tamaa za fedha na maisha mazuri badala yake wafanye kazi kwa bidii na kutanguliza uzalendo mbele

Huku mmoja kati ya viongozi dini,Dk,Askofu ,Solomoni Masangwa wa Kanisa la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati (KKKT) alisisitiza amani na upendo ikiwemo kuwaombea viongozi wa serikali.


Sehemu ya Gwaride la Askari wa Jeshi la Akiba Mapema Leo kwenye bustani ya mnara wa Mashujaa Jijini Arusha
Sehemu ya Askari waasisi wa vita na Mashujaa wakifuatilia sherehe hizo


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: