Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana akifungua mkutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD)Mapema Leo Jijini Arusha 

Na Ahmed Mahmoud


SERKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kwa kushirikiana na Wadau  wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera Sheria Taratibu na kanuni kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ikiwemo biashara ya Utalii ambapo imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara hiyo.

Kwa Muktadha huo Serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza mfumo wa pamoja wa biashara baina ya wadau wa Utalii ikiwa ni lengo la kupata huduma zote sehemu moja za tozo kodi na malipo yote ya sekta hiyo(One stop Shop) ili sekta hiyo ichangie kikamilifu katika uchumi

Akiongea wakati akifungua mkutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD)Jijini Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt,Hazra Pindi Chana amesema kwamba maagizo aliyotoa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 13 wa baraza la taifa la biashara TNBC jijini Dodoma alituagiza tukutane na sekta binafsi hususani sekta ya Utalii kujadili mapendekezo na mageuzi ya sera sheria kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara hiyo.

Amesema kwamba serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya Utalii ili ichangie kikamilifu katika uchumi na maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla pia dhamira hii
inaenda sambamba na uendelezaji wa malengo a kimkakati ya mpango wa Tanzania The Royal Tour katika kukuza Utalii kadhalika na Uhifadhi wa
maliasili na malikale zetu.

Awali akiongea akati akimkaribisha Waziri Chana  katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Eliaman Sedoyeka alisema kwamba kupitia wizara hiyo wamejipanga kuongeza juhudi kubwa za kuutangaza Utalii duniani ikiwa ni ishara ya kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan alieafanya kwa vitendo kuandaa Filamu ya Royal
Tour.

Amesema Pamoja na sekta hiyo kuathiriwa na uwepo wa janga la Uviko 19 sanjari na vita baina ya mataifa ya Urusi na Ukrein bado wizara itaendelea kupanua soko la utalii kufikia malengo ya watalii milion 5
mwaka 2025.

Kwa Upande wake Mshauri wa Mazingira ya Uwekezaji IFC Anita Kundy amesema kwamba Tangu 1956, IFC imewekeza zaidi ya dola bilioni 2.8 katika miradi zaidi ya 260 katika nchi 89 na zaidi ya nusu ya uwekezaji huu katika nchi nyingine. Nchini Tanzania, tumewekeza pia katika hoteli jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Dunia na Baraza la Utalii, kila dola inayotumika kwa usafiri na utalii inazalisha zaidi ya dola tatu za pato la kiuchumi.Zaidi ya wafanyakazi milioni 100 wameajiriwa katika sekta hii duniani kote, na mapato ya utalii yanachangia mtiririko wa fedha zaidi kwa nchi zinazoendelea kuliko mtiririko wote wa misaada kutoka kwa wafadhili wa kigeni.

 Alisema IFC inafuraha kuunga mkono na kusapoti kufikiwa kwa malengo muhimu ya serikali ya awamu ya 6 ya kuifanya Tanzania kama kivutio cha utalii na uwekezaji. Kwa miaka sitini, IFC, mwanachama wa Benki ya Dunia, imefanyakazi na sekta binafsi kwenye kuleta masuluhisho yaliyoleta mabadiliko chanya kijamii na kiuchumi.

Kwa Mujibu wa Kundy amesema imefanikisha hili kwa kuunda masoko mapya,kuhamasisha wawekezaji binafsi, na kutoa msaada wa kitaalamu. IFC
inawekeza katika hoteli na utalii kwa sababu ya faida zake kubwa za maendeleo, hasa kwa nchi za kipato cha chini na zilizoathiriwa na migogoro.

Wadau wa sekta ya Utalii wakifuatilia Mada mbalimbali Wakati wa M
kutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD) Mapema Leo Jijini Arusha 
Wadau wa sekta ya Utalii wakifuatilia Mada mbalimbali Wakati wa Mkutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD) Mapema Leo Jijini Arusha 

Picha ya Pamoja ya Wadau wa Utalii wakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hazra Pindi Chana pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Prof. Eliaman Sedoyeka Mapema Leo Jijini Arusha




Picha ya Pamoja ya Wadau wa Utalii wakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hazra Pindi Chana pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Prof. Eliaman Sedoyeka Mapema Leo Jijini Arusha
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: