Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Gilbert Kalima akiongea na viongozi wa Baraza la Wazazi mkoa wa Arusha Mapema Jana Jijini Arusha
Sehemu ya viongozi wa Baraza la Mkoa la Jumuiya ya Wazazi Arusha wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotolewa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na viongozi wa Chama hicho mkoa wa Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Na Ahmed Mahmoud

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Gilbert Kalima Amewataka wale wote wenye sifa za kugombea kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na kuacha kuendelea kutumiwa Kwa maslahi ya viongozi wachache wanaotaka madaraka.


Aidha ameeleza kwamba viongozi wapya wa matawi wa Jumuiya hiyo tunataka kuona jumuiya ikimarika kiuchumi kwa kila mkoa kuhakikisha iongoze na ijipange kuimarika kiuchumi.


Kalima Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na viongozi wa Baraza kuu la mkoa wa Arusha katika ukumbi wa CCM mkoa Jijini Arusha ambao aliitaka Jumuiya ya Wazazi kuwa ya mfano kwa tuwe uadilifu na wmfano kwa Jumuiya zengine katika kukiimarisha chama na kujenga Utulivu kwa kuimarisha Amani miongozo na kanuni sanjari na kujiimarisha uchumi.


Watu wanaenda kushawishiwa anayeshawishiwa Kwa maslahi ya mtu ajitafakari au yule anayeambiwa akachukuwe fomu ujue amefilisika na ajiulize mara mbili kama anafaa kwa nafasi hiyo kwani huu sio muda wa kuwabeba watu wasiotufaa.


"Sisi viongozi wa Jumuiya na chama tuwe wa mfano Arusha na idhihirishe kuwa Jumuiya hii ni ya mfano kwa kujenga uchumi ndani ya Jumuiya kuifanya kuimarika kiuchumi kuendana na Msingi ya kuigwa na Jumuiya zengine"


Tukienda kwenye ahadi tulizitoa kwa wananchi inakaiwa Jumuiya kukaa na kuona serikali inatekeleza ilani tukianza kulaumiana sisi kwa sisi hilo sio Lengo la chama chetu.


"Hivi sisi wanaarusha tumetafakari uzinduzi wa Royal tour kwa nini imezinduliwa hapa tutafakari vizuri kwanini Arusha kwa mustakabali wa Maendeleo na kukuza Amani Utulivu na mshikamano kuelekea katika uchumi Imara wa mkoa huu"


Tuhakikishe tunaulizia na kufuatilia Ilani ya uchaguzi kukagua na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ili kujua Yale tulioahidi yamefanyika ili tuendelee kushuka dola. 


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen Amewataka  Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kamamieni kanuni na miongozo katika kukisimamia Chama kwa utaratibu wa vikao na sio kwenye mitandao.


Amewataka watumie mitandao kujenga chama na Jumuiya zake na tuache kuweka Siri zetu mitandaoni za kukibomoa chama chetu kwani sisi nyie dira ya utendaji na Msingi wa mafanikio yaliopo 
"
Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mussa Matoroka akiongea kwenye mkutano wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Arusha 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akiongea katika Mkutano wa Baraza la Mkoa la Jumuiya ya Wazazi lililoboreshwa Jana Jijini Arusha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Hezron Mbise akiongea katika Baraza la Jumuiya hiyo Mapema Jana Jijini Arusha
Meza kuu wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Gilbert Kalima kwenye Mkutano wa Baraza la Jumuiya hiyo mkoa wa Arusha Mapema Jana Jijini Arusha


Msingi Mkubwa uwe ni kukiimarisha chama na sio vingine Jumuiya ya Wazazi ipo salama haina makando kando naziomba Jumuiya zengine pamoja na chama kuiga mfano huu"

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: