Na,Jusline Marco;Arusha

Wabunge wa Kikanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana jijini Arusha kujadili nafasi na mchango wa mwanamke Barani Afrika katika ngazi za uongozi bora.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wanawake wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Fatma Ndangiza ameyasema hayo katika mkutano wa wawakilishi wa wabunge wa kikanda na wadau wa masuala ya wanawake  iliofanyika jijini Arusha.

Mhe.Ndangiza amesema maazimio yatakayotoka katika mkutamo huo yatasaidia kuweka kipaumbele kwa wanawake ili kuwafanya kuwa na mchango kwa maendeleo ya taifa kwa kuwa na wanawake wengi katika ngazi za maamuzi.

Aidha amesema baadhibya mila na desturi kandamizi zimekuwa zimekuwa kichocheo kikubwa na vikwazo kwa watoto wa kike na wanawake kuweza kushiriki kwenye maendeleo ya kijamii.


Awali akifungua mkutamo hio kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson,Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mtwara Mhe.Anastazia Wambura amesema wanawake wa Afrika wanapaswa kuwa watafutaji wa nafasi za uongozi wa kisiasa katika nchi zao.

Mhe.Wambura amesema lengo na madhumuni ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu baina ya nchi na nchi katika masuala ya uongozi wa kisiasa kwa kila mmoja kutoa uzoefu wake katika ongezeko la idadi ys viongozi wanasiasa wanawake.

"Nikitoa mfano wa nchi ya Rwanda wao wapo mbele yetu kwa asilimia 64 ya wanawake kuwa bungeni ukilinganisha na nchi yetu ya Tanzania ambapo  asilimia 37 tu ya wanawake ndiuo wapo bungeni,kwa hiyo tukibadilishana uzoefu tukajua wenzetu walifanya nini wakafikia kiwango hicho na sisi tutafanya hivyo ili kuongeza kiwanho hicho japo najua wapo miongoni mwetu  walio chini ya kiwango chetu."Alisema Mhe.Wambura

Ameongeza kuwa katila mkutano huo pia watatoa kwa pamoja kuangalia nini kifanyike ili kuweza kuhakikisha wanawake wa Afrika wanapata nafasi ya uongozi katika siasa.


Naye Mbunge kutoka Congo DRC, Mhe.Agness Sadiki katika mkutano huo ameeleza kufurahishwa na ushiriki wake ambapo amewapongeza wanawake kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Zambia kwa kupiga hatua katika kumshirikisha mwanamke kwenye ngazi za uongozi.

Sambamba na hayo ameeleza kuwa kupitia mikakati ambayo itapitishwa katika mkutano huo itapelekea wao kama nchi ya Congo DRC kuwaomba viongozi wao wakuu waliotia sahihi mikataba mbalimbali ikiwemo wa protocal wa Maputo kuwashirikisha wanawake kwenye kila kitu ambacho kinaleta amani ili kutoa usawa katika jinsia zote.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: