Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais -Idara ya Mazingira Bi.Catherine Bamwenzaki akizungumza katika warsha ya Mafunzo kuhusu Mchango wa Taifa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ambapo warsha hiyo imefanyika leo Juni 24,2022 katika ukumbi wa mkutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Mkoani Morogoro.Mratibu wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Vijijini kwa kutumia mfumo wa Ikolojia Dkt.James Nyarobi akiwasilisha mada katika warsha ya Mafunzo kuhusu Mchango wa Taifa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ambapo warsha hiyo imefanyika leo Juni 24,2022 katika ukumbi wa mkutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Mkoani Morogoro.

Afisa Mazingira-Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi.Asia Akule akiwasilisha mada katika warsha ya Mafunzo kuhusu Mchango wa Taifa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ambapo warsha hiyo imefanyika leo Juni 24,2022 katika ukumbi wa mkutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Mkoani Morogoro.

Mtaalamu wa mabadiliko ya Tabianchi Bw.Abbas Kitogo akiwasilisha mada katika warsha ya Mafunzo kuhusu Mchango wa Taifa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ambapo warsha hiyo imefanyika leo Juni 24,2022 katika ukumbi wa mkutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais -Idara ya Mazingira Bi.Catherine Bamwenzaki akipata picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa mazingira katika warsha ya Mafunzo kuhusu Mchango wa Taifa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ambapo warsha hiyo imefanyika leo Juni 24,2022 katika ukumbi wa mkutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Mkoani Morogoro.

************************

Tanzania imeweka wazi mikakati mbalimbali itakayosaidia kupunguza uzalishaji wa gesijoto kwa asilimia 30 hadi asilimia 35 ifikapo mwaka 2030 ikiwemo kushirikisha makundi yote kwenye jamii ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Tanzania ni mwanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) na ni miongoni mwa nchi zilizowasilisha Mchango wake wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Nationally Determined Contribution (NDC) kwenye Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, Julai 30, 2021.

Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira, Bi Catherine Bamwenzaki amesema hayo leo Juni 24, 2022 mkoani Morogoro katika warsha ya mafunzo kuhusu mchango wa Taifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa waandishi wa habari

Bamwenzaki amesema shabaha hiyo ya kupunguza uzalishaji gesijoto itategemea uwezo kiuchumi ambapo kiasi Sh19.2 bilioni zinategemewa kutekeleza mpango huo.

Amesema NDC ni mwitikio wa kimataifa wa nchi wanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi, kama ilivyofafanuliwa katika Kifungu cha 4 (2) cha Makubaliano ya Paris, ambacho kinazitaka kila nchi mwanachama kuandaa na kuwasiliana mchango wake wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambao inakusudia kuifikia.

“Malengo makuu ya kimataifa ya NDCs ni kuchangia katika kupunguza athari na kuimarisha ustahimilivu wa muda mrefu wa mabadiliko ya tabianchi; kuchangia katika juhudi za kupunguza uzalishaji wa gesi joto ili kufikia lengo kuu la Mkataba ambalo ni kupunguza uzalishaji wa gesi joto kwenye anga katika kiwango ambacho hakitaleta madhara kwenye mfumo wa hali ya hewa,” amesema Bamwenzaki.

NDC imeainisha hatua za kuchukuliwa kwenye eneo la kuhimili athari na pia kupunguza uzalishaji wa gesijoto ambapo imeainisha sekta za kipaumbele zikiwemo sekta za kilimo, mifugo, misitu na wanyamapori.

“Maoneo mengine yalipoweka kipaumbele ni pamoja na nishati, mazingira ya bahari na ukanda wa pwani na uvuvi (bahari na maziwa), maji na usafi wa mazingira, utalii, makazi ya binadamu, afya, miundombinu, majanga na masuala mtambuka ikiwemo jinsia, tafiti, fedha na teknolojia,” amesisitiza Bamwenzaki.

Katika kupunguza gesijoto, sekta za kipaumbele ni pamoja na nishati, misitu, usafirishaji na taka. Sekta hizi ndiyo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa gesijoto kwa sasa na zina fursa kubwa ya kuchochea na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.

Amesema hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na kuandaliwa kwa Mpango Kabambe wa kimakakati, maandalizi ya mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya tabianchi, na Sera ya Mazingira, 2021 iliyozinduliwa Februari, 2022.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mtaalam wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Abbas Kitogo amesema wanashirikiana na Serikali ya Tanzania kufanikisha shabaha hiyo ya kupunguza uzalishaji wa gesijoto ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kwa sasa wanatekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo kubuni na kutekeleza miradi ya nishati safi na salama ikiwemo matumizi ya majiko banifu na mkaa mbadala kwa kushirikisha makundi mbalimbali kwenye jamii.

Amesema kwa sasa Tanzania inachangia asilimia 0.36 ya gesijoto yote inayozalishwa duniani.

Naye Mratibu wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi vijijini kwa kutumia mifumo ya ikolojia (EBARR), Dk James Nyarobi amesema EBARR ni kielelezo cha utekelezaji wa NDC unaojikita katika kuwajengea uwezo wananchi hasa wa vijijini kutumia vifaa na nyenzo visivyoleta uchafunzi na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo unatekelezwa katika wilaya tano za Tanzania zikiwemo Kishapu, Mvomero, Mpwapwa, Simanjiro na Kaskazini A visiwani Zanzibar.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: