CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeendesha mafunzo ya
kuwajengea uwezo mafundi sanifu zaidi ya 25 kutoka Taasisi mbalimbali za
Serikali nchini kutumia vifaa vya kisasa vya kuongeza ubora wa bidhaa
zitokanazo na mimea dawa ili ziweze kushika soko la ndani na nje na kuongeza
pato la mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla.
Akizungumzia mafunzo hayo Mkuu wa Mradi wa Mradi wa Matumizi ya
Ubunifu ,uvumbuzi na teknolojia mbalimbali katika kuboresha bidhaa za mimea
dawa ili kuboresha Maisha (GRILI) Dkt. Faith Philemon Mabiki kutoka SUA amesema
mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wataalmu hao kutoka zaidi ya taasisi
saba nchini namna ya kutumia vifaa vya kisasa vya uchunguzi lakini pia kuweza
kufanya marekebisho pale vifaa hivyo vinapoharibika.
“Ili bidhaa yoyote itoke kwenye soko la ndani iingie kwenye soko la
kikanda na kimataifa swala la ubora ni muhimu sana na unapozungumzia ubora
huwezi kukwepa matumizi ya vifaa vya uchunguzi na hawa tuliowakuleta hapa ndio
wahusika wakuu wa kutumia vifaa hivyo kwenye taasisi zao nchini , hivyo
tunahitaji wawe na uwezo wa kuvitumia lakini pia kuvifanyia matengenezo
vinapoharibika” alisema Dkt. Mabiki.
Dkt. Mabiki ameongeza kuwa lengo linguine ni kutaka wafahamiane na
kuweza kushirikiana wenyewe kwa wenyewe katika ya taasisi moja na taasisi
nyingine katika kusaidiana pale mmoja anapopata changamoto katika kufanya kazi
hizo na hata pale inapoharibika waweze kusaidiana.
Amesema kupitia yote hayo wnataka kuboresha ubora wa bidhaa za mimea
dawa ili zishike soko na kuleta kipato kwa wat una taifa lakini pia
kuwahakikishia watumiaji usalama na kufikia malengo ya taifa yam waka 2025.
Mradi wa GRILI umewezesha kununu na kufunga vifaa vya kisasa katika
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo vyenye uwezo wa hali ya juu ya kupima ubora
wa bidhaa zitokanazo na mimea dawa na bidhaa zingine ili kuhakikisha usalama wa
bidhaa kwa watumiaji.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanaendeshwa na wawezashaji wane kutoka Chuo kikuu cha Copenhagen cha nchini Denmark ambao ni Prof. Christian Janfelt, Prof. Nickolaj Petersen,Prof. Bjarne Styrishave na Keneth Pedersen na yanafadhiliwa na Shirika la maendeleo la Denmark DANIDA kupitia Mradi wa GRILI katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo.
Post A Comment: