Loliondo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka washiriki wa zoezi la uwekaji alama za mipaka kujituma ili kazi ya uwekaji alama hizo katika maeneo ya Loliondo na Ngoronhoro iishe kwa wakati.

IGP Sirro ameyasema hayo katika ziara yake aliuoifanya kwenye eneo la Loliondo na Ngorongoro kwa ajili ya kujionea zoezi linaloendelea la uwekaji alama za mipaka, ambapo ameeleza kuridhishwa na kasi iliyopo.

Sirro amesisitiza wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na serikali katika uamuzi huu wenye lengo la kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi ambapo amewataka wananchi hao  kutokubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote  na wala wasikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasioitakia mema taifa.





Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amemhakikishia IGP Sirro kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imejipanga kuhakikisha kuwa zoezi linaendeshwa kwa hali ya utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.

Ikumbukwe kuwa Serikali haichukui Ardhi bali imetoa Ardhi kwa wakazi wa Loliondo ambapo awali eneo la pori tengefu lililokuwa limehifadhiwa lilikuwa ni Kilomita za mraba 4000,serikali kwa kutambua uhitaji na shughuli za kijamii Loliondo imetoa eneo la Kilomita za mraba 2500 na kuwapatia Wananchi na kufanya eneo lililobaki kwa ajili ya pori tengefu kuwa ni Kilomita za mraba 1500 .

Hata hivyo alama za mipaka ambazo zinawekwa Loliondo sio za kuwafukuza wakazi bali ni kutenganisha eneo lililobakizwa kwa ajili ya uhifadhi na lile lililorudishwa kwa Wananchi wa Loliondo .



Share To:

JUSLINE

Post A Comment: