Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amekipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa bunifu ambazo zinalenga kutatua changamoto katika Jamii.


Mkuu huyo wa Mkoa ameelekeza baadhi ya bunifu za Chuo hicho zipewe maeneo katika mkoa wa Dodoma ili zifanyike kwa vitendo.


Mtaka amesema  hayo baada ya kutembelea banda la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika   maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayoendelea katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.


Mhe Mtaka amesema lengo la bunifu ni kuziondoa kwenye mfumo wa mifano na kuziweka kwenye uhalisia.


Naye Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila leo ametembelea maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayoendelea katika viwanja vya Jamhuri mkoani Dodoma ambapo amekipongeza Chuo kwa kazi za nzuri ya bunifu.


Kauli mbiu katika maonesho hayo ni 

"Kuinua Ubora wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa ajili ya Nguvukazi Mahiri Tanzania"


Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, 

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

7.06.2021


Share To:

Post A Comment: